Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa
PS3, Dk Conrad Mbuya (kushoto) akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo bahasha iliyo na majina ya Wilaya mbili zitakaanzo anza utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya seklta za Umma (PS3) Mkoani Kigoma. Mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Misaada la Kimataifa la Marekani (USAID).
Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo akionesha bahasha hiyo kwa washiriki. Kushoto ni Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa
PS3, Dk Conrad Mbuya na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Mrisho Mrisho.
Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo akitangaza majina ya Halmashauri Mbili za Wilaya ambazo zitaanza katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi wa PS3 mkoani Kigoma. Halmashauri za Uvinza na Buhigwe zilipita.
Washiriki wakiwepo wakuu wa Wilaya wakishangilia kwa uteuzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mlindoko akifuatilia mkutano huo.
Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa
PS3, Dk Conrad Mbuya (kushoto) akizungumza namna utekelezaji utakavyofanyika. Wengine ni Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo (katikati) na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, Mrisho Mrisho.
Mkurugenzi wa shughuli za mikoa wa
PS3, Dk Conrad Mbuya alisema mradi utaanza mara moja utekelezaji wake
na kwa kuanzia wataanza na mifumo ya tehama kwa kuangalia hali ya miundombinu
na kuiboresha.
Mkaguzi
Mkuu wa Ndani kutoka Idara ya Mkaguzi Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Alphonce
Muro akijadili jambo na Mkurugenzi Msaidizi Utumishi, Kajura wakati wa mkutano huo.
Washiriki wakiwa katika mkutano huo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


No comments:
Post a Comment