Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa anatoka kwenye Wodi ya Sewahaji katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili na kurejea nyumbani mara baada
ya kuruhusiwa baada ya kupata nafuu. Mama Janeth Magufuli alikuwa amelazwa
hospitalini hapo tangu tarehe 9 Novemba 2016.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Raymond Mwenesano, Mkuu wa Idara
ya Wagonjwa wa nje na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kurejea
nyumbani baada ya kupata nafuu.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru
Dkt. Edward Ngwalle, Daktari wa Rais mara baada ya kuruhusiwa kutoka
hospitalini hapo na kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.
. Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt.
Benard Kepha ambaye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura na ajali katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka na kurejea
nyumbani mara baada ya kupata nafuu. Picha
na IKULU
No comments:
Post a Comment