Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashimu Komba (katikati), akikata utepe kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo, kuashiria kupokea madawati 80 yaliyotolewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa Shule ya Msingi ya Kibasila Dar es Salaam.
Ofisa Mistu wa Wilaya ya Temeke, Fredrick Umilla (kulia), akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi madawati.
Meneja wa TFS Wilaya ya Temeke, Francis Kiondo (kulia), akitoa taarifa kwa mgeni rasmi.Meneja wa TFS Wilaya ya Temeke, Francis Kiondo (wa pili kulia), akimkabidhi mgeni rasmi, Hashim Komba hati ya makabidhiano wa madawati hayo. Kutoka kushoto ni Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Betha Minga na Mwakilishi wa Meneja wa Kanda ya Mashariki wa TFS, Mohamed Lyandama.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes wakishiriki kupanda mti. Kulia ni Masha Hassan na Yahaya Hamza.
Na Dotto Mwaibale
WAFANYAKAZI wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Temeke wametakiwa kuendelea kuwa waadilifu katika kazi zao za kila siku ili kujiepusha na vitendo vya rushwa kutoka kwa watu wanaojihusisha na uharamia wa mali asili ya nchi.
Mwito huo ulitolewa Dar es Salaam jana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashim Komba kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo wakati akipokea madawati 80 yenye thamani ya sh. 6,370, 000 yaliyotolewa na TFS wilaya ya Temeke kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa madawati wilayani humo.
"Kwa hali halisi ninayoiona hapa ofisini kwenu najua ninyi ni waadilifu mnaviepuka vitendo vya rushwa endeleeni kusimamia kazi yenu ili kulinda mali asili ya taifa" alisema Komba.
Komba alisema kuwepo kwa magunia ya mkaa na mbao katika ofisi hiyo zilizokamatwa na kielelezo tosha kuwa hakuna vitendo vya rushwa vinavyofanywa na maofisa wa ofisi hiyo.
Komba amewaomba TFS kuendelea kuchangia madawati ili kumuunga mkono
Rais Dk. John Magufuli ya kuhakikisha wanafunzi wanasoma bure na katika mazingira bora ikiwemo kukaa kwenye madawati.
Akitoa taarifa fupi wakati wa kukabidhi madawati hayo Meneja Wakala wa Huduma za Misitu Wilaya Tanzania (TFS) Wilaya ya Temeke, Francis Kiondo alisema wakala tangu kuanzishwa kwake wamepata mafanikio makubwa kupitia utekelezaji wa mpango mkakati wa kwanza wa miaka mitatu 2011 -2014 ambapo sasa wanaelekeza nguvu katika kutekeleza mpango mkakati wa pili wa miaka mitatu 2014 hadi 2016.
Alisema katika kutekeleza majukumu yake wakala imepata changamoto za uvamizi wa maeneo ya misitu kwa ajili ya kilimo, ufugaji, makazi, ukataji miti, uchimbaji madini na uchomaji moto misitu.
Alisema ili kukabiliana na changamoto hizo inatakiwa kuongeza watumishi na vitendea kazi na kujenga vituo katika kila msitu wa hifadhi na kuweka mabango ya tahadhari.
Kiondo alisema kuwa wakala umetayarisha mpango bora wa usimamizi wa uhifadhi wa misitu na moja ya mikakati iliyopo kwenye mpango huo ni kupanda hekta 185,000 za miti kwa mwaka kwa kushirikiana na wadau ili kuziba pengo la mita za ujazo 19.5 milioni kwa mwaka za timbao hadi kufikia miaka 2030.
No comments:
Post a Comment