Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene akiangalia madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Ineke Busineker. (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Ineke Busineker akikabidhi sehemu ya madawati 3500 kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene.
xxxxxxxxxxxxxxxxxx
WAKUU wa Mikoa na Maofisa Elimu wa mikoa ambayo haijamaliza tatizo la uhaba wa madawati mashuleni, wametakiwa kukamilisha mchakato huo kabla ya kufunguliwa shule Januari mwakani, vinginevyo watawajibishwa.
Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Ineke Busineker akikabidhi sehemu ya madawati 3500 kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene.
xxxxxxxxxxxxxxxxxx
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, wakati akipokea msaada wa madawati 3500 yenye thamani ya Sh. Mil. 300 kutoka Benki ya NMB.
Hafla hiyo ilifanyika Ofisi za Tamisemi jijini Dar es Salaam, ambako Waziri Simbachawene aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Geita, Mwanza, Kigoma, Mara, Dodoma, Rukwa na Simiyu, ambayo inapaswa kumaliza tatizo hilo.
“Mikoa hiyo haijamaliza tatizo la madawati mashuleni. Tunawaomba, kabla ya kufungua shule Januari mwakani, wamalize tatizo hili, vinginevyo nitawahesabu kama wameshindwa na nitawasilisha taarifa zao kwa Rais,” alisema Simbachawene.
Waziri Simbachawene aliipongeza NMB kwa kushirikiana na Serikali katika kumaliza changamoto zinazoikabili Sekta ya Elimu, huku akizitaka taasisi, mashirika na kampuni zingine, kuiga mfano wa benki hiyo.
“Katika hili NMB wanapaswa kuigwa na kila mmoja, imekuwa sehemu ya elimu ya Tanzania na changamoto zake na tunajisikia faraja kupokea msaada huu wa madawati 3500, yenye ubora na thamani ya Sh. Mil. 300.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Ineke Busineker, alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya kiasi cha Sh. Bil. 1.5, ambacho ni asilimia moja ya pato lao, walilolitoa kusaidia Sekta ya Elimu nchini.
Alibainisha kuwa, NMB itaendelea kusaidia sekta ya elimu nchini, kwani inaamini kuelimisha watoto ni kuielimisha jamii na wateja wajao wa benki hiyo na kwamba nia ni kuboresha na kutanua wigo wa wanafunzi kupenda elimu.
No comments:
Post a Comment