HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 20, 2017

ZIARA YA MAJALIWA BABATI NA MBULU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sukari na nishati ya kuni inayotengenezwa kwa kutumia makapi ya miwa inayokamuliwa katika kiwanda cha sukari cha Manyara wakati alipotembelea kiwanda hicho Februari 19, 2017.  Kuni hizo zina ubora unaofanana na ule wa makaa ya mawe na hutumika zaidi katika mitambo inayotumia  nishati ya kuni. Kulia ni Waziri wa  Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na kulia kwa Waziri Mkuu, ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya mstaafu, Mama Sanka baada  ya kuwasili  kwenye makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara  mjini Babati akiwa katika ziara ya mkoa huo, Februari 19, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sanamu ya binadamu  wakati alipotembelea moja ya darasa  la Chuo cha Uuguzi katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu, Februari 20, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu, Rosemary Mshama  (kulia)  wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti cha hospitali hiyo Februari 20, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wahatzabe wakati alipowasili kwenye hospitali ya Haydom kuanza ziara ya  wilaya ya Mbulu, Februari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Pages