Na Talib Ussi Zanzibar
Wakati Wazanzibari wakijiandaa na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Mfumko Bidhaa za vyakula vimeonekana kupanda bei kutoka 6.4 March nakufikia 7.1 kwa mwezi April huku unga wa sembe na Sukari zikiongoza.
Hayo yamebainika leo wakati Kaimu wa Afisi ya Mtakwimu mkuu wa Serikali Khamis Msham akizungumza na waandishi wa habari huko Afisini kwake Mwanakwerekwe Unguja.
Msham alieleza kuwa hali hiyo imetokana mvua kubwa zinazoendelea kunyesha ambapo hakuna mazao mapya na wazalishaji kutumia hakiba iliyopo.
Alieleza unga wa sembe ulikuwa 1800 kg march na kufikia 2000 kwa mwezi wa april 2017 huku sukari ikitoka 1500 kutoka april 2016 na kufikia 2000 kwa mwaka huu wa 2017.
Kwa upande wa Mchele wa mbeya umepanda kutoka 2300 mwaka jana hadi kufikia 2500 April 2017 huku mchele unaogizwa kutoka nchi za nje ukibakia katika bei hile ya zamani.
Sambamba na hilo hakuna mfumko kwa bidhaa za mafuta ya kupikia pamoja na Saruji ambayo inatoka Tanzania Bara.
Imekuwa jambo la kawaida kwa Zanzibar bidhaa kuwa juu huku serikalii wakidai hawana uwezo wa kuzia kutokana kuwepo kwa soko huria.
“Sasa wafanyabiashara wachukua bidhaa zao wenyewe na wao ndio wajua gharama ni ngumu kudhibiti upandishaji wa bei kiholela, labda tuwe tuna viwanda nchini” alieleza Msham.
No comments:
Post a Comment