Mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko
Tanzania kutoka jijini Mwanza Pildas Emmanuel kushoto akipeana mikono
ya shukrani na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven baada ya
kumkabidhi fedha zake jijini Dar es Salaam kama sehemu ya ushindi wa
Bahati Nasibu ya Biko inayoendelea nchini Tanzania na kugawa mamilioni
kwa washindi wake.
Mshindi wa Mwanza atua Dar kubeba mamilioni yake
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHINDANO
la mchezo bahati na nasibu la Biko Ijue Nguvu ya Buku, limemkabidhi
mshindi wake wa wiki ya tatu ya Sh Milioni 10, ambaye ni Pildas
Emmanuel, anayeishi jijini Mwanza baada ya kutangazwa mshindi wa wiki
katika droo iliyochezeshwa Jumapili iliyopita.
Makabidhiano
ya fedha hizo yalifanyika jijini Dar es Salaam sambamba na kumfungulia
akaunti ya benki ya NMB kwa ajili ya kuingiza fedha hizo kwa mshindi
huyo aliyejitambulisha kama mjasiriamali wa vileo jijini Mwanza
Tanzania.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na baadhi ya wataalam wa benki
ya NMB kwa ajili ya kumpa elimu ya kifedha mshindi huyo, Meneja Masoko
wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alisema sasa Biko limekolea na
wameendelea kumwaga fedha kwa kila mshindi wao, akiwamo Emmanuel
aliyeletwa kwa Ndege kwa ajili ya kumkabidhi fedha zake.
Alisema kila siku wamekuwa wakilipa zawadi za papo kwa papo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh 1,000,000, pamoja na zawadi kubwa ya wiki ya Sh Milioni 10 kwa kila mshindi wao, huku wakiwa wameshalipa kiasi hicho kwa washindi wawili ambao ni Christopher Mgaya, Nicholaus Mlasu ambao wote wameshapokea fedha zao.
“Biko limekolea na linaendelea kuwapatia utajiri wananchi wa Watanzania wanaothubutu kucheza Biko kwa kufanya miamala kwenye simu zao za Tigo, Vodacom na Airtel, ambao ni mchezo wa ujumbe mfupi wa maandishi kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kumalizia namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456, huku tiketi moja ikipatikana kwa sh 1000.
“Na kila Sh 1000 itakayolipwa itakuwa na nafasi mbili ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya wiki ya kuwania Sh Milioni 10, huku mshiriki akiruhusiwa kucheza kuanzia Sh 1000 au zaidi ambapo kucheza mara nyingi zaidi ndio kujiweka katika nafasi nzuri ya ushindi,” Alisema Heaven na kuwataka Watanzania waendelee kucheza Biko ili wavune mamilioni ya Biko.
Naye Emmanuel alisema kwamba amefurahishwa na huduma zote alizopewa na Biko ikiwamo ya kumpa fedha zake katika benki ya NMB pamoja na kumleta jijini Dar es Salaam kwa ndege kutoka Mwanza jambo ambalo halijawahi kumtokea katika maisha yake.
“Ingawa nimepata fedha nyingi ambazo sijawahi kuzishika tangu nizaliwe, pia nimeingia kwenye historia kwa sababu na mimi nimepanda ndege kwa mara kwanza huku fedha zote zikilipwa na Biko, hivyo ni kampuni nzuri na mchezo wao ni mzuri kutokana na malipo ya ushindi kulipwa haraka,” Alisema Emmanuel na kuwataka Watanzania waendelee kucheza Biko.
Emmanuel aliwasili jijini Dar es Salaam Jumatatu akitokea jijini Mwanza ikiwa ni siku moja baada ya kutangazwa mshindi na Balozi wa Biko, Kajala Masanja katika droo iliyoshuhudiwa pia na Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.
Meneja Masoko wa Biko Tanzania,
Goodhope Heaven kulia, akishuhudia jinsi mshindi wao wa Sh Milioni wa
bahati nasibu ya Biko, Pildas Emmanuel anavyofurahia baada ya kumkabidhi
fedha zake mapema wiki hii jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment