HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2017

SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Na Talib Ussi, Zanzibar

Wakati Dunia ikijitayarisha kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani, Zanzibar imepata ghofu ya kuongezeka maradhi ya mripuko, kutokana na uharibifu mkubwa wa Mazingira

Jumuiya ya kupambana na mabadiliko ya tabianch ZACCA imesema  visiwa vya Zanzibar vinakabiliwa na mabadiliko ya tabianch  yatayosababisha upoteaji wa misiti ya asili,kuongezeka kwa maradhi ya miripuko na kupotea kwa rasilimali ya mchanga.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Amina Yussuf Kashorowa akizungumza na  Waandishi wa habari  ikiwa ni  shamrashamra ya kuadhimisha  Siku ya mazingira duniani  ambayo kwa Tanzania inatarajiwa kuadhimisha tarehe 5  huko Musoma Butiama.

Aliahamisha kuwa uharibifu wa mazingira  unapelekea  kuongeza kasi  ya athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo uchimbaji mchanga,ukataji misitu kwa matumizi ya mkaa na kuni,uharibifu wa vyanzo vya maji ikiwemo ujenzi na ulimaji katika maeneo ya vyanzo vya maji na kusababisha mafuriko.

Hata hivyo Amina alieleza  licha yajuhudi mbalimbali  zinazochukuliwa kupambana na matatizo hayo  lakini bado  yanashika kasi  na kuhatarisha mustakabali wa zanzibar kimazingira.

Aidha alieleza kwamba ni   wakati muafaka  kwa jamii kuwa na uelewa juu ya tatizo hilo na kutafuta njia bora  za kilimo na ufugaji kwani mabadiliko hayo  yameathiri sana mifumo ya maisha ikiwemo kilimo,ufugaji,nishati,utalii pamoja na afya.

Aidha Zacca  imeishauri Wizara ya fedha ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kutenga  fedha zaidi kusaidi miradi ya jamii  ya kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi ili kupunguza kasi kwa jamii kuharibu mazingira kama ukataji miti ovyoo kwaajili ya mahitaji yao.

Mwenyekiti huyo alieleza ya kuwa  ipo haja SMZ  kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo  kuweka nguvu zao katika kuwaelimisha jamii juu ya athari hizo kwani tafiti zilizofavywa na idara ya misitu na maliasili zisizorejesheka inaonesha  Zanzibar  inapoteza hekta 500 kwa kila mwaka kutokana  wananchi wa Zanzibar wanategemea  kuni na mkaa kwa asilimia 97.

No comments:

Post a Comment

Pages