JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
_____________
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
________________________
Kufuatia barua aliyopokea
Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai kutoka kwa Mwenyekiti Prof. Ibrahim
Haruna Lipumba na Kaimu Katibu Mkuu Mhe.
Magdalena Hamisi Sakaya (Mb) wa Chama cha Wananchi (CUF), Mheshimiwa Spika
angependa kuwaarifu Watanzania wote kwamba amejiridhisha kuwa Wabunge hao
wamefukuzwa Uanachama kulingana na taratibu za Chama hicho na hivyo wamekosa
sifa za kuendelea na Ubunge. Wabunge hao ni: -
1.
Mhe.
Severina Silvanus Mwijage, (MB);
2.
Mhe.
Saumu Heri Sakala, (MB);
3.
Mhe.
Salma Mohamed Mwassa, (MB);
4.
Mhe.
Riziki Shahari Mngwali, (MB);
5.
Mhe.
Raisa Abdallah Mussa, (MB);
6.
Mhe.
Miza Bakari Haji, (MB);
7.
Mhe.
Hadija Salum Ally Al-Qassmy, (MB); na
8.
Mhe.
Halima Ali Mohamed, (MB).
Hivyo, kwa mamlaka
aliyonayo kwa kuzingatia kifungu cha 67(1)(b) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ya Mwaka 1977 kikisomwa pamoja na kifungu 37(3) cha Sheria ya
Uchaguzi Sura 343 kama ilivyojadidiwa Mwaka 2015, Mheshimiwa Spika ametangaza
nafasi hizo kuwa wazi na pia kumuandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili
aendelee na hatua zinazostahili kujaza
nafasi hizo kwa Mujibu wa Sheria
na Taratibu zilizopo.
Imetolewa na:
Ofisi ya Spika,
S. L. P. 941,
DODOMA.
26
Julai, 2017
No comments:
Post a Comment