Bodi
ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
limefanya mabadiliko kidogo katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara kama ifuatavyo.
Michezo
ambayo imefanyiwa mabadiliko ni kati ya Tanzania Prisons na Majimaji ya
Songea; Azam FC na Simba, Njombe Mji na Young Africans; Mtibwa Sugar
na Mwadui FC ambayo sasa itachezwa Septemba 6, 2017.
Pia
tarehe hiyo ya Septemba 6, mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Lipuli
na Stand United; Singida United na Mbao; Kagera Sugar na Ruvu Shooting
wakati Mbeya City na Ndanda FC .
Michezo
mingine ambayo imesogezwa hadi Septemba 11, 2017 ni kati ya Azam na
Kagera Sugar wakati Mbao na Tanzania Prisons utachezwa Septemba 21,
mwaka huu.
Kadhalika
mechi nyingine zitachezwa Oktoba 11, mwaka huu ni kati ya Mbao na Azam
FC; Kagera Sugar na Mwadui; Mbeya City na Ruvu Shooting; Ndanda na
Singida United.
Tarehe
hiyo pia Oktoba 11, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Njombe Mji na
Simba; Mtibwa na Tanzania Prisons; Lipuli na Majimaji wakati Stand
United na Young Africans watacheza Oktoba 12, mwaka huu.
Novemba
15, 2017 Mbao itacheza na Young Africans; Kagera na Mbeya City; Stand
United na Azam; Mwadui na Ruvu Shooting; Singida na Njombe Mji; Lipuli
na Tanzania Prisons; Mtibwa Sugar na Majimaji wakati Novemba 16, Ndanda
itacheza na Simba.
……………………………………………………………………………… …………
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment