Klabu
ya Simba inapenda kuwajulisha wanachama na mashabiki wake kuwa,Golikipa wake wa
kimataifa,Said Mohamed Nduda amepata matatizo ya goti ambayo yamempelekea
kueleka India kwa ajili ya matibabu.
Nduda
aliumia mazoezini wakati timu ikijiandaa kuelekea mchezo dhidi ya Yanga wiki
ilipita,Matibabu hayo yatamuweka mchezaji huyo nnje kati ya wiki nne hadi sita
kabla ya kujiunga tena na wenzake kwa ajili ya mazoezi na anatarajiwa kuondoka
nchini mwishoni mwa wiki hii.
Klabu
pia inayofuraha ,kuwaambia kuwa wachezaji wake John Bocco na Haruna Niyonzima
,ambaye alipata majeraha madogo juzi wameshaanza mazoezi na wenzao hii leo.
Huku
pia Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi wa muda mrefu naye anatarajiwa kuanza
mazoezi siku chache zijazo baada ya madaktari kuthibitisha uzima wa afya yake.
Mwisho,Klabu
inaufahamisha umma wa watanzania kupitia vyombo vya habari kuwa taarifa zote
rasmi za klabu ya Simba zitakuwa zikitolewa katika mfumo na barua hii(Heading
paper)
Pia
Klabu inawaomba washabiki wake kote nchini kuendelea kuiunga mkono timu yao ili
iendelee kufanya vizuri kwenye ligi kuu iliyoaanza wikiendi iliyopita.
Imetolewa
na Mkuu wa Habari na Mawasiliano
Haji.S.Manara
SIMBA
NGUVU MOJA
No comments:
Post a Comment