HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 23, 2017

Tigo yatoa zawadi kwa mara ingine

Meneja  Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama akimkabidhi simu aina ya Tecno S1, Ally Mwaisemba,  mmoja kati ya washindi 113 wa promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi jijini Dar Es Salaam leo. Jumla ya washindi 219 wamejishindia simu hizo nchi nzima.
  Meneja  Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama akimkabidhi simu aina ya Tecno S1, Justina Lyimo, mmoja kati ya washindi 113 wa promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi jijini Dar Es Salaam leo. Jumla ya washindi 219 wamejishindia simu hizo nchi nzima.
Washindi wa promesheni ya Tigo Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao za simu aina ya Tecno S1. Jumla ya washindi 219 wamejishindia simu hizo nchi nzima.
 
Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, imetoa zawadi za simu papaso aina ya Tecno S1 kwa wateja wake 219 ambao wamejishindia simu hizo kupitia promosheni inayoendelea ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi.

Akizungumza kwenye hafla ya kutoa zawadi kwa washindi 113 kutoka Dar es Salaam jana, Meneja Biashara wa kampuni hiyo Suleiman Bushagama alisema kwamba hii ni wiki ya pili katika utoaji wa zawadi, ambapo kwa wiki ya kwanza washindi 120 walizawadiwa simu hizo.

“Tofauti na promosheni nyingine ambapo wateja wachache tu wanapata zawadi, Tigo inatoa simu moja ya Tecno S1, kila saa kwa masaa 24 kila siku ya wiki kwa muda wote wa kampeni hii ya kusisimua, hadi sasa tuna jumla ya washindi 339,” alisema Bushagama.

Kwa mujibu wa Bushagama, promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe, Ujaziwe Zaidi inamuwezesha kila mteja wa Tigo kuwa na nafasi ya kujishindia simu anapoongeza salio, hii inaenda sambamba na kupata zawadi za papo hapo za kifurushi cha muda wa hewani, muda wa kuperuzi au kifurushi cha meseji kila anapoongeza salio.

“Washindi wa simu ya smartphone ya Tecno S1 pia watafurahia mawasiliano ya bure ya simu kwa mwaka mmoja. Zawadi nyingine anazoweza kushinda mteja ni pamoja na bonasi ya bure kwenye huduma ya sauti, data na ujumbe mfupi wa maneno SMS kulingana na matumizi ya mteja husika, "aliongeza Bushagama.

Kwa mujibu wa Tigo, jumla ya simu za mkononi 720 zipo tayari kunyakuliwa katika promosheni inayoendelea sasa ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi. Wateja wanaweza kushinda simu za mkononi kila saa kirahisi kwa kuongeza muda wa maongezi wa Tigo kupitia kadi za kukwangua, e-pin au TigoPesa, ambapo namba yao ya simu itaingia kwenye droo ya nafasi ya kushinda moja ya simu za mkononi zinazoshindaniwa kila saa , ya kila siku kwa siku saba za wiki.

Aliendelea kuongeza kuwa Waratibu wa Biashara na Masoko wa Tigo tayari wamejiandaa kukabidhi simu za smartphones kwa washindi wengine wa droo ya wiki hii waliopatikana kutoka Dodoma, Morogoro, Pwani, Kilimanjaro, Rukwa, Shinyanga na Pemba.

"Kama kawaida, Tigo inasikiliza na kuitikia mahitaji ya wateja wake, na sasa tunawapatia zawadi kemkem kama njia mojawapo ya kuwashukuru kwa kuendelea kutumia bidhaa na huduma zetu bora. Nachukua fursa hii kuwakumbusha wateja wote wa Tigo kwamba zawadi ni nyingi na wote wanaoshiriki wanashinda zawadi, kwa hiyo wachangamkie fursa hii ya kusisimua ya kuvuna zawadi kupitia promosheni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi ", alisema Bushagama.

No comments:

Post a Comment

Pages