Msajili wa Mashirika yasiyo ya
kiserikali Bw. Marcel Katemba akitoa
ufafanuzi wa kazi ya uhakiki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuhimiza wadau
kuitikia zoezi hilo katika muda uliowekwa na Serikali alipokutana na waandishi wa
habari leo hii katika ukumbi wa Mikutano ya Wizara UDOM, Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini, WAMJW
Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WAMJW
Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambayo inajukumu la kusajili, kuratibu na kufuatilia
uendeshaji wa shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini imeamua
kuongeza muda wa siku 16 kwa Mashirika ambayo bado hayajahakiki taarifa zake kwa Msajili wa Mashirikka yasiyo
ya Kiserikali kukamilisha uhakiki huo.
Akizingumza na
waandishi wa Habari Mjini Dodoma leo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba
Nkinga amesema kuwa kumekuwa na mwitikio mkubwa wa Mashirika yasiyo ya
kiserikali kuja kuandikisha taarifa za asasi zao katika vituo mbalimbali vya
usajili vya kanda.
Bibi Sihaba
ameongeza kuwa Serikali ina nia njema ya na siyo mbaya kama watu wanavyohisi
katika utekelezaji wa zoezi hili la uhakiki linaloendelea nchi nzima katika
vituo vya Kanda tano (5), na lengo ni la zoezi ni kutambua takwimu halisi ya Mashirika
yanayofanya kazi ili kuweka utaratibu mzuri wa kutambua mchango wa kila asasi
katika kuhudumia jamii katika nyanja mbalimbali.
“Niwaombee
wadau wetu watumie muda huu tuliouongeza vizuri kwa kujitokeza kwa wingi
kufanya uhakiki wa Mashirika yao na wale wenye changamoto tutawaelekeza namna
bora ya kuzitatua”alisema Bibi Sihaba.
Aidha Msajili
wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Bw. Marcel Katemba amewahikikishia wadau wa
mashirika yasiyo ya kiserikali nchini kuwa hakuna tatizo katika zoezi la
uhakiki wao na ni muhimu sana kujihakiki ili kujiwekea mazingira mazuri ya
kufanya kazi zao kwa uhuru na uwazi.
“
Niwahakikishie wadau wetu kuwa zoezi hili ni muhimu sana kwenu na kwetu pia
katika namna ya kuboresha utendaji kazi wetu”alisema Bw. Katemba.
Naye Katibu wa
Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini Bw. Ismail Suleiman ameishukuru
Serikali kuwa kuandaa na kuratibu zoezi la uhakiki wa mashirika hayo na
kuwaomba wamiliki wa mashirka yasiyo ya kiserikali nchini kujitokeza kuhakiki
mashirika yao.
“Niwaombe
wamiliki wa Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini tuendelee kujitokeza kwa
wingi tuje tuhakiki mashirika yetu ili tuondokane na usumbufu mara baada ya
kumalizika kwa kuda wa uhakiki ulioongezwa”alisema Bw. Ismail.
Zoezi la
uhakiki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini lilizinduliwa na katibu Mkuu Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Agosti 21,2017 na uhakiki
huo ulitekelezwa kwa muda wa wili mbili mpaka Septemba 04,2017.
Hata hivyo
kutokana na sababu za kijiografia na mwitikio mkubwa wa mashirika kutaka
kuhakikiwa ikaamuliwa kuongeza kwa muda wa siku 16 mpaka Septemba 20 mwaka huu,
ambao ndio utakuwa mwisho wa uhakiki.
No comments:
Post a Comment