Mwamuzi
wa kimataifa, Elly Sasii atakuwa mwamuzi katika mchezo wa kirafiki kati
ya Taifa Stars ya Tanzania na Zebras ‘Pundamilia’ ya Botswana
utakaofanyika kesho Jumamosi Septemba 2, mwaka huu.
Katika
mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kwenye Uwanja wa
Uhuru, Dar es Salaam waamuzi wasaidizi watakuwa Soud Lillah (Line 1) na
Frank Komba (Line 2) wakati mwamuzi wa akiba (Forth Official) atakuwa
Israel Nkongo.
Mchezo
huo utaanza saa 10.00 jioni unaochezwa chini utaratibu wa kalenda ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambako Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepanga Watazamaji waingie uwanjani kwa
kiingilio cha Sh 10,000 kwa Jukwaa Kuu na Sh 5,000 kwa mzunguko.
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga leo Ijumaa amezungumza na wanahabari
kwenye Ukumbi wa Hosteli ya TFF, Karume jijini Dar es Salaam ambako
amethibitisha kwamba kikosi chake kiko imara kwa mapambano.
Kwa
upande wa Kocha wa Botswana, David Bright amesema yeye ni kocha mpya na
amejitahidi kuteua timu mpya yenye mchanganyiko wa vijana na wazoefu
aliokuja nao kuwajaribu kwa nyota wa Kitanzania.
Taifa
Stars iko kambini na nyota wake akiwamo Nahodha Mbwana Samatta (KRC
Genk/Ubelgiji), Elias Maguli (Dhofar FC/Oman), Abdi Banda (Baroka
FC/Afrika Kusini), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya),Farid Mussa (CD
Tenerif/Hispania) na Simon Msuva (Difaa El Jadidah ya Morocco).
Wengine
ambao wako kambini Hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam
ni makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani
Kabwili (Young Africans).
Pia
wamo Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao
FC), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto
Nyoni (Simba SC).
Viungo
ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Mzamiru Yassin (Simba SC),
Said Ndemla (Simba SC), Shiza Kichuya (Simba SC), wakati Washambuliaji
ni Raphael Daud (Young Africans), Kelvin Sabato (Azam FC) na Emmanuel
Martin (Young Africans).
……………………………………………………………………..…… ………..……
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment