Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam-Tanzania, Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, imetoa zawadi za
simu papaso aina ya Tecno S1 kwa wateja wake 720 ambao wamejishindia simu hizo
kupitia promosheni iliyofikia tamati ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi.
Akizungumza kwenye hafla ya kutoa
zawadi kwa washindi 120 kutoka Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano wa
kampuni hiyo Woinde Shisael alisema kwamba hii ni wiki ya nne na ya mwisho katika
utoaji wa zawadi.
“Tofauti na promosheni
nyingine ambapo wateja wachache tu
wanapata zawadi, Tigo inatoa simu moja ya Tecno S1, kila saa kwa masaa 24 kila
siku ya wiki kwa muda wote wa kampeni hii ya kusisimua, kwa leo tumemalizia
zoezi maana tumekabidhi simu zote 720,” alisema Shisael.
Kwa mujibu wa Shisael, promosheni
ya Tigo Jaza Ujazwe, Ujaziwe Zaidi inamuwezesha kila mteja wa Tigo kuwa na
nafasi ya kujishindia simu anapoongeza salio, hii inaenda sambamba na kupata
zawadi za papo hapo za kifurushi cha muda wa hewani, muda wa kuperuzi au
kifurushi cha meseji kila anapoongeza salio.
“Tunafurahia kuona kwamba
tumekuwa sehemu ya safari ya wateja wetu ambao wamejishindia simu za smartphone
aina ya Tecno S1 ambao pia watafurahia mawasiliano ya bure ya simu kwa mwaka
mmoja.
Zawadi nyingine ambazo mteja alikuwa anaweza kujishindia ni pamoja na
bonasi ya bure kwenye huduma ya sauti, data na ujumbe mfupi wa maneno SMS
kulingana na matumizi ya mteja husika, "aliongeza Shisael.
Kwa mujibu wa Tigo, simu hizo
zitawawezesha washindi kupata taarifa mabalimbali , kuchukua picha na pia
kuzitumia katika matumizi mbalimbali.
Wateja waliweza kushinda simu za mkononi kila saa kirahisi kwa kuongeza muda wa maongezi wa Tigo kupitia kadi za kukwangua, e-pin au
TigoPesa, ambapo namba yao ya simu ilikuwa inaingizwa kwenye droo ya
nafasi ya kushinda mojawapo ya simu za mkononi zilizoshindaniwa kila saa
, ya kila siku kwa siku saba za wiki.
"Kama kawaida, Tigo
inasikiliza na kuitikia mahitaji ya
wateja wake, na sasa tumewapatia zawadi kemkem kama njia mojawapo ya
kuwashukuru kwa kuendelea kutumia bidhaa na huduma zetu bora. Nachukua fursa
hii kuwashukuru wateja wote wa Tigo kwa kuwa pamoja nasi ambapo wengi wao
wamejishindia zawadi mbalimbali,", aliongeza Shisael.
Kwa upande wake, Amon Mkude
ambaye ni mkaazi wa Mbezi Msakuzi jijini Dar es Salaam, alisema kwamba
hakuamini alipopigiwa simu kwamba kajishindia simu, “yaani sikuamini, nilidhani
matapeli, ila nimeamini baada ya kupewa simu hii, nawashukuru sana Tigo kwa
zawadi hii,” aliongeza Mkude.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akimkabidhi simu aina ya Tecno S1 mmoja kati ya washindi 120 waliojishindia simu kwenye promosheni ya mwisho ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi, Sarah Lema, mkazi wa Tabata, jumla ya washindi 720 wamejishindia simu nchi nzima . Hafla hiyo ilifanyika Duka la Tigo Manzese jijini Dar es Salaam
Meneja
Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akimkabidhi simu aina ya Tecno S1
mmoja kati ya washindi 120 waliojishindia simu kwenye promosheni ya
mwisho ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi, Amour Haji, mkazi wa Mbagala,
jumla ya washindi 720 wamejishindia simu nchi nzima. Hafla hiyo
ilifanyika Duka la Tigo Manzese jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment