HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 12, 2017

WANANCHI WAOMBWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA KUFICHUA VITENDO VYA UKIUKWAJI WA MAADILI KATIKA UTUMISHI WA UMMA

 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Lambert Chialo, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu uzingatiaji wa Maadili kwa Watumishi wa Umma katika utendaji kazi. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais-Utumishi, Mary Mwakapenda.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MAADILI KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Utangulizi 

Utumishi wa Umma una wajibu wa kuleta ustawi kwa wananchi kwa kutoa huduma, ili kuweza kufikia lengo hilo la Serikali, ni dhahiri kuwa Utumishi wa Umma hauna budi kuendeshwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu; kutanguliza maslahi ya taifa na kuzingatia Maadili katika utendaji wa kila siku. Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 (Kifungu cha 34) kinaipa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR-MUU) mamlaka ya kukuza na kufuatilia uzingatiaji wa Maadili katika Utumishi wa Umma.
Katika kutekeleza jukumu hilo, OR-MUU imekuwa ikiendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika suala la usimamizi wa Maadili kwa kutoa miongozo inayosimamia Maadili, kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miongozo hiyo, kutoa mafunzo na elimu kwa umma. 

Maadili ya Utumishi wa Umma yamejengeka katika misingi mikubwa mitatu ambayo ni kuzingatia Utaalamu, Uaminifu na Uwajibikaji. Misingi hii, ndio imeunda Kanuni za 8 Maadili ambazo:-
 Kutoa Huduma Bora;  Utii kwa Serikali;
1
 Bidii ya Kazi;
 Kutoa Huduma bila Upendeleo;  Kufanya kazi kwa Uadilifu;
 Kuwajibika kwa Umma;
 Kuheshimu Sheria; na
 Matumizi sahihi ya Taarifa. 


Hata hivyo, pamoja na kuwepo na Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma na miongozo mingine inayosimamia uadilifu kumekuwa na changamoto ya kujenga Utumishi wa Umma ambao unazingatia Uadilifu kutokana na baadhi ya watumishi kutozingatia miongozo hiyo.
Changamoto Katika Ukuzaji wa Maadili
Waajiri wamekuwa wakikumbana na changamoto katika kukuza na kusimamia Maadili kutokana na baadhi ya watumishi kuwa na mienendo ifuatayo:-

 Utoro kazini:- baadhi ya watumishi wamejenga mazoea ya kutofika kazini bila sababu ya msingi kinyume na Kanuni 57 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003 na Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma. Tutambue kwamba kutofika kazini kwa zaidi ya siku tano bila sababu ya msingi ni kosa na mtumishi anapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu na adhabu yake ni kufukuzwa kazi, punguzo la mshahara/kushushwa cheo. 

Taarifa ya miaka 10 ya Tume ya Utumishi wa Umma 2004-2014 imeonyesha kuwa kati ya mwaka 2008-2013, Watumishi wa Umma 2755 walichukuliwa hatua za kinidhamu ambapo watumishi 1,142 walifukuzwa kazi kwa makosa mbalimbali ambapo makosa ya utoro kazini ilikuwa asilimia 54, ubadhirifu wa mali ya umma asilimia 20 na makosa mengineyo asilimia 26. 

Matumizi Mabaya Taarifa za Serikali: - hii inatokana na watumishi wachache kutuma taarifa za siri na za kawaida kwa watu ambao sio walengwa wa taarifa hizo. Hivi karibuni tumeshuhudia taarifa za siri zikitumwa katika mitandao ya kijamii kama whatsapp, blog na mingeneyo kinyume na Kanuni za Maadili ambapo inasisitizwa kuwa
2
na matumizi sahihi ya taarifa. Kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa Na. 3 ya mwaka 1970 na marekebisho yake, Ibara ya 5(a)&(b) , adhabu ya uvujaji wa siri ni Kifungo kisichozidi miaka 20. 

Ifahamike, lengo la Serikali si kuficha taarifa kwa wadau ila taarifa zinazotolewa zinapaswa kupelekwa kwa ambao wanapaswa kupokea taarifa hizo (walengwa). Aidha utoaji wa taarifa unapaswa kufuata utaratibu wa utoaji wa taarifa na zipate idhini kwa Mtendaji wa Taasisi kabla ya kupelekwa kwa wadau. 

Matumizi mabaya ya Ofisi: - baadhi ya watumishi wamekuwa wakitumia nafasi walizonazo kwa manufaa yao binafsi na sio kwa umma, mfano kughushi taarifa ambazo zina maslahi kwao na matumizi mabaya ya vifaa vya serikali. Mfano wakati wa zoezi la uhakiki ilibainika watumishi walioghushi vyeti vya Elimu na Taaluma ili kujipatia ajira, kupanda vyeo au kubadilisha kazi. Serikali itaendelea kuhakiki taarifa hizo kila inapohitajika kwa kuwa upo uwezekano wa watu kuendelea kudanganya pamoja na jitihada za serikali zinazoendelea. 

Ubadhirifu wa Mali ya Umma
Taarifa ya miaka 10 Tume ya Utumishi wa Umma 2004-2014 imeonyesha kuwa kulikuwa na Mashauri ya Jinai 2,322 kati ya mwaka 2004-2013 ambapo asilimia 60 ya Mashauri hayo yalikuwa ni ubadhirifu wa mali ya umma, asilimia 16 ilikuwa rushwa na asilimia 24 mengineyo. 

Vitendo vinavyoaibisha Utumishi wa Umma kama uvaaji wa mavazi yasiyofaa kinyume na Waraka wa Mavazi Na.3 wa mwaka 2007 kwa watumishi wa Umma. Wapo watumishi ambao hawazingatii waraka huo kwa kuvaa nguo zinazobana, fulana, nguo zinazoonyesha sehemu za mwili na mavazi mengine yasiyofaa. Aidha watumishi wanapaswa kufahamu uvaaji wa fulana unaruhusiwa tu wakati wa shughuli maalumu zinazotambulika na Serikali na kwa zile Taasisi ambazo zimejiwekea utaratibu wa kuvaa sare rasmi za fulana kwa baadhi ya siku za kazi wanaruhusiwa kufanya hivyo. 

3
Hitimisho
Usimamizi wa Maadili ni suala shirikishi hivyo kila mmoja katika nafasi yake anapaswa kuchukua hatua ili kuleta mabadiliko na hatimaye kuboresha utoaji wa huduma.
Kutokana na Maadili kuwa suala mtambuka, inasisitizwa Viongozi na wasimamizi wa kazi kuendelea kuelimisha suala la Maadili na kuhakikisha watumishi wanaishi na kuzizingatia Kanuni hizo kwa wao wenyewe kuwa mfano. 
Pili, Watumishi wa Umma wakumbuke wajibu wao kwa wananchi kwa kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo. Watumishi waache kufanya kazi kwa mazoea na kutimiza wajibu wao kwa wananchi.  

Mwisho, kwa kuwa suala la Maadili linaanzia katika ngazi ya familia, wananchi wanaombwa kushiriki kikamilifu katika kufichua vitendo vya ukiukwaji wa Maadili katika Utumishi wa umma kwa kutoa taarifa kwa Mamlaka zinazohusika na kutumia madawati ya malalamiko yaliyo katika Taasisi za Umma. Pia, endapo kuna taarifa na uthibitisho wa watumishi ambao bado wanaendelea kutumia vyeti ambavyo sio vyao au hawapo katika vituo vyao vya kazi bila sababu ya msingi (utoro) huku wakiendelea kupokea mshahara wa Serikali mnaombwa kuwasilisha taarifa hizo kwa Katibu Mkuu – Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa hatua. 
IMETOLEWA NA OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA
TAREHE 12 SEPTEMBA, 2017
 

No comments:

Post a Comment

Pages