WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa msaada wa sh. milioni 10 ili
kumuwezesha Bw. Ernest Masenga kutatua changamoto zinazomkabili.
Bw. Masenga alikuwa msanii wa muziki wa dansi ambaye sasa
anasumbuliwa na maradhi ya miguu. Pia makazi anayoishi si salama yanahitaji
kukarabatiwa.
Waziri Mkuu ametoa msaada huo leo (Jumatatu, Septemba 11, 2017)
katika makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar Es Salaam.
Ametoa msaada huo baada ya kuguswa na hali ya maisha ya msanii
huyo aliyemuona kupitia kipindi maalumu kilichoonyeshwa na TBC Sempemba, 5,
2017. Kipindi hicho kiliongozwa na Bw. Godfrey Nago.
“Nawaomba Watanzania wenzangu tumsaidie mwezetu ili aweze kuishi
vizuri kwa sababu sanaa yake imesaidia katika kuelimisha na kuburudisha umma .”
Kwa upande wake Bw. Nago ambaye amepokea
msaada huo kwa niaba ya Bw. Masenga amesema atahakikisha anasimamia vizuri
fedha hizo ili zitumike kama ilivyokusudiwa.
Pia Bw. Nago amesema anamshukuru Waziri Mkuu kwa kuwaunga mkono
na kutoa msaada huo kwa sababu ameonesha kwamba Serikali inawajali wananchi
wake na TBC itaendelea kuwaomba wadau mbalimbali wajitokeze na kumsaidia msanii
huyo.
Naye Mjomba wa msanii huyo
Bw. Kanuti Mloka ambaye ameiwakilisha familia amemshukuru Waziri Mkuu kwa
msaada huo kwa kuwa familia imeshindwa kumsaidia Bw. Masenga kutokana hali duni
ya maisha waliyonayo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, SEPTEMBA 11, 2017.
No comments:
Post a Comment