HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 29, 2017

CCM YAZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA UDIWANI KIJICHI LEO, KUSILAWE ASEMA CCM ITASHINDA UDIWANI KATA ZOTE TATU DAR

 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe akimnadi mgombea wa CCM katika uchaguzi wa marudio wa Udiwani Kata ya Kijichi, Eliasa Mtalawanje,Temeke Dar es Salaam, leo. Akizungumza amesema CCM itashinda Udiwani kata zote tatu ambako uchaguzi unarudiwa mkoani Dar es Salaam. Kata zingine ni Saranga na Mbweni.
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe akiwasili kwenye Uwanja wa mkutano kuzindua kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya Kijichi, leo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Almishi Hazal
 Wananchi na wana CCM wakishangilia wakati Kusilawe na viongozi wenzake wakiingia Uwanjani.
 Mtalawanje akitroti baada ya kutambulishwa na Mwenyekiti wa Wazee wa CCM Temeke.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Wilaya ya Temeke Mohammed Mbonde, akizungumza baada ya kukaribishwa jukwaani kusalimia.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Temeke Mohammed Mbonde, akipongezwa na Mgombea Udiwani kata ya Kijichi Eliasa Mtalawanje baada ya kutoka jukwaani kusalimia.
 Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo akisalimia wananchi kwenye mkutano huo, na kuzungumza kuhusu umuhimu wa wananchi kumchagua mgombea wa CCM Udiwani kata ya Kijichi.
 Mbunge wa Mbagala Issa Mangungu, akisalimia wananchi kwenye mkutano huo, na kuzungumza kuhusu umuhimu wa wananchi kumchagua mgombea wa CCM Udiwani kata ya Kijichi.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Almishi Hazal akisalimia wananchi na kumkaribisha Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, kuhutubia mkutano huo na kumtambulisha mgombea wa CCM wa Udiwani Kata ya Kijichi. 
 Baadhi ya wananchi kwenye mkutano huo
 Viongozi wa Baraza la wazee Temeke wakiwa kwenye mkutano huo
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe akihutubia mkutano huo
 Kusilawe akisisitiza jambo
 Vijana wa CCM wakimshangilia Kusilawe
 Msimamizi wa uchaguzi wa CCM makao makuu Mzee Kazidi (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Wilaya ya Temeke Almishi Hazal. katikati ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam
 Mzee Kazidi akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Kuslawe.
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe akimnadi mgombea wa CCM katika uchaguzi wa marudio wa Udiwani Kata ya Kijichi, Eliasa Mtalawanje,Temeke Dar es Salaam, leo  
 Kisha akamkabidhi mgombea huyo ilani ya CCM
 Kusilawe akimkabidhi ilani mgombea huyo
 Mgombea akionyesha ilani baada ya kukabidhiwa.
 Eliasa Mtalawanje akifafanua jambo kwa makini
 Wananchi wakimshangilia mgombea huyo
 Mgombea huyo akiendelea kuomba kura kwa wananchi 
Mgombea wa CCM katika uchaguzi wa marudio wa Udiwani Kata ya Kijichi, Eliasa Mtalawanje,Temeke Dar es Salaam, akiondoka uwanjani mwishoni mwa mkutano. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

No comments:

Post a Comment

Pages