Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akisikiliza maelezo kuhusu namna ya kuikabili Sumu Kuvu kutoka kwa Msaidizi wa Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi ya
Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania Bi
Eveline Massam wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akipokea zawadi ya Boga kutoka kwa Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mara baada ya kutembelea Banda la Taasisi hiyo wakati wa
maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika
uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Afisa Habari na Uelimishaji Jamii kutoka Mamkaka ya Chakula na Dawa Bi Robert Feruzi (Kulia) akimuelezea Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa jinsi Mamlaka hiyo inavyofanya kazi wakati alipotembelea Banda la Taasisi hiyo kwenye
maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika
uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Meneja Mwendeshaji wakulima wadogo kutoka Benki ya wakulima (TADB) Ndg Joseph Mabula (Kulia) akimuelezea Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (KUshoto) jinsi inavyofanya kazi wakati alipotembelea Banda la Benki hiyo hiyo kwenye
maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika
uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akionyesha Mvinyo uliotengenezwa na wajasiriamali wadogo wakati alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali kwenye
maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika
uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akikagua mashine mbalimbali katika Banda la kampuni ya POLY MACHINERY CO.LTD kwenye
maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika
uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa akikagua baadhi ya vyakula vilivyohifadhiwa kwenye vifungashio kwenye
maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika
uwanja wa CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Na
Mathias Canal, Geita
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa
ameishauri Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA)
kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wakulima nchini kuhusu kadhia ya Sumu Kuvu.
Alisema kuwa elimu
hiyo inatakiwa kutolewa katika maeneo mbalimbali nchini ili wananchi waweze
kutambua namna bora katika uandaaji wa mashamba wakati wa msimu wa kilimo ikiwa
ni pamoja na kuhakikisha mashamba hayashambuliwi na magugu wala wadudu
waharibifu.
Naibu Waziri ametoa
ushauri huo wakati akizungumza na Msaidizi
wa Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki
(IITA) nchini Tanzania Bi Eveline Massam mara baada ya kutembelea Banda
hilo wakati wa Maonesho ya 36 ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Katika Uwanja wa CCM
Kalangalala Mjini Geita kuanzi Octoba 10 mpaka Octoba 16.
Dkt Mwanjelwa
alisema kuwa wakulima wengi nchini wanalima pasina kufahamu taratibu za kilimo
cha kisasa jambo ambalo linapelekea mazao yao kuathiriwa na wadudu husani Sumu
Kuvu na kupelekea uduni wa mavuno.
Alisema kuwa endapo
Taasisi hiyo ya (IITA) itaongeza nguvu ya utoaji elimu kwa wakulima kwa
kushirikiana na wataalamu wa Wizara ya kilimo, wananchi watanufaika na kilimo
chao ikiwa ni pamoja na kuwa na mavuno mengi.
Alisema Sumu Kuvu
inahatarisha afya za watumiaji wa mazao mbalimbali ya chakula na biashara,
kwani chakula na malisho ya mifugo iliyo athiriwa na sumu kuvu hupunguza
uzalishaji huku mazao yenye kiwango kikubwa cha Sumu Kuvu zaidi ya kiwango
kinachoruhusiwa kutekelezwa au yanauzwa kwa bei ya chini.
Aidha, zipo athari
za moja kwa moja kwani endapo binadamu au mnyama atakula chakula chenye malisho
yenye kiwango kikubwa cha Sumu Kuvu anaweza kupoteza maisha.
Kwa upande wake Msaidizi wa Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi ya
Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania Bi
Eveline Massam alisema kuwa Sumu Kuvu huzalishwa wakati fangasi aina ya
Aspergillus anaposhambulia mbegu shambani/ghalani.
Aliongeza kuwa
Ukuaji wa fangasi na athari za sumu kuvu husababishwa na mabadiliko ya hali ya
hewa (Ukame wa ongezeko la joto), Mbinu duni za kilimo kabla na baada ya kuvuna
mazao kwa mfano; ukaushaji hafifu wa mazao punde yanapovunwa, na uhifadhi duni
wa mazao ghalani na wadudu waharibifu.
Sumu Kuvu ni aina
za kemikali za sumu zinazozalishwa na aina ya Ukungu au Fangasi wanaoota kwenye
mbegu za nafaka kama vile mahindi, mbegu za mafuta kama karanga, jamii ya kunde
na pia mazao ya mizizi. Pia sumu Kuvu hupatikana katika bidhaa za mifugo kama
vile maziwa, mayai na nyama pale ambapo chakula kinacholiwa na mifugo kitakuwa
kimechafuliwa na sumu hizo.
Sambamba na hayo pia Naibu waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa alitembelea Banda la Benki ya Maendeleo ya kilimo, Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe na Banda la Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA).
Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani hufanyika kila mwaka kuanzia Octoba 10 mpaka Octoba 16 ambapo kwa mara kwanza yalianza mwaka
1981. Hivyo maadhimisho ya mwaka huu ni ya 36 na yanasherehekewa kwa pamoja na
maadhimisho ya miaka 72 ya kuanzishwa
kwa FAO tarehe 16 Oktoba, 1945.
No comments:
Post a Comment