Kamati
mpya ya Uongozi ya Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) inafanya kikao chake cha kwanza Alhamisi,
Oktoba 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Moja
ya ajenda katika kikao hicho ni kuteua Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi,
na kamati nyingine mbalimbali.
TPLB
ilifanya uchaguzi Jumapili, Oktoba 15 mwaka huu na kupata uongozi mpya chini ya
Mwenyekiti wake Clement Sanga.
Viongozi
wengine waliochanguliwa ni Shani Mlingo (Makamu Mwenyekiti) na wajumbe Hamisi Madaki,
Ramadhani Mahano, Almasi Kasongo na Egdar Chibura.
Boniface
Wambura
Ofisa
Mtendaji Mkuu
Bodi
ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
No comments:
Post a Comment