HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 23, 2017

MSAMA ATIKISA KARIAKOO, AKAMATA VIFAA, KAZI FEKI


Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama, akiongoza operesheni ya kukamata vitendea kazi vinavyotumika kuingiza nyimbo, video kwenye simu na kurudufu isivyo halali CD za kazi za wasanii, katika mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).

 Alex Msama akifungua moja ya kompyuta zilizokuwa zinatumika katika  kuingiza nyimbo na video katika simu katika eneo la Kariakoo.

Askari Polisi akiwa katika Operesheni ya kukamata wafanyabiashara haramu wa kazi za wasanii.

Na Mpiga Picha Wetu

KAMPUNI ya Msama Auction Mart ya jijini Dar es Salaam, leo mchana imemfanya msako mkali wa kushtukiza dhidi ya ya wafanyabiashara wanaodurufu kazi za wasanii mbalimbali katika mitaa ya Kariakoo na viunga vyake jijini Dar es Salaam

Msako huo uliodumu takribani kwa saa mbili kuanzia majira ya saa saba mchana chini ya Askari wa Jeshi la Polisi kutoka Kituo cha Kati na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ulifanikiwa kukamata kompyuta na mashine zipatazo 50 za kufyatulia kazi feki.

Mbali ya vifaa hivyo ambavyo vinashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Kati cha jijini Dar es Salaam, pia watu wapatao 17 wanashikiliwa kwa kujihusisha na kazi hiyo haramu ambayo imekuwa ikiwanyima wasanii husika mapato.

Akizungumzia opearesheni hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama, alisema kazi ndio kwanza imeanza na kusema itakuwa endelevu sio tu kwa jiji la Dar es Salaam, bali katika mikoa yote.

“Kazi ndio kwanza imeanza, tulianza kwa kuwaonya kwa maneno matupu, kwamba waache kazi hii haramu kwa sababu ni kuwanyonya wasanii, pia kuinyima Serikali mapato yake halali, lakini hawakusikia,” alisema Msama.

Alisema kinachosikitisha ni kwamba, wasanii mbalimbali wawe wa muziki wa injili ama bongo feleva hata dansi, wamekuwa wakikosa mapato stahiki kutokana na kazi zao kuuzwa bei chee mitaani na wajanja wa kudurufu.

Msama ametoa wito kwa vijana wenye kujihusisha na kazi hiyo haramu, kuacha na kutafuta kazi nyingine halali kwa sababu chini ya utawala wa Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli, biashara ya njia za mkato, hatari.

Alisema kwa sasa kazi hiyo itaendelea katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam hadi watakapojiridhisha kuwa tatizo hilo limekwisha, hivyo itakuwa zamu ya msako huo kuhamia katika mikoa mbalimbali nchini.

Mbali ya kuwaonya vijana kuachana na biashara hiyo haramu,Msama ametoa wito kwa wananchi mbalimbali kuacha kununu kazi feki japo huuzwa kwa bei ya chini, wanunue kazi halali zenye nembo ya TRA.

Alisema kwa kufanya hivyo, mwananchi atakuwa amemwezesha msanii husika kupata ujira kulingana na jasho lake, pia Serikali kupata kodi yake kwa maendeleo ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Pages