HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 24, 2017

Kizimban kwa kumiliki magar 19

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imempandisha kizimbani Ofisa msaidizi wa forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA),Jennifer Mushi na kumsomea mashtaka mawili ikiwamo ya kumiliki magari 19 yenye thamani ya sh 197,601,207 yasiyolingana na kipato chake.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu mkazi mkuu, Huruma Shahidi, wakili wa serikali Vitalis Peter alidai kati ya 21/3/2016 na 30/6/2016 katika maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam,akiwa mfanyakazi wa TRA, mshtakiwa huyo alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake, kinyume na sheria.

Alidai kuwa magari hayo ni, Toyota Ra4, Toyota dyna truck, Toyota viz, Suzuki carry,Toyota ipsum,toyota wish,Toyota mark ll,Toyota regiusage,Toyota estima,Toyota Alex,Toyota Noah,Toyota crown,Toyota hiace,Toyota estima,Toyota passo, Suzuki carry, yote yakiwa na thamani ya 197,601,207

Katika Shtaka la pili, anadaiwa kuwa kati ya 21/3/2012 na 30/3/2016 maeneo ya Dar es salaam akiwa mwajiri wa TRA aliishi maisha ya kipato cha juu (kifahari) tofauti na kipato chake yenye thamani ya sh. 333,255,556.24 na .

Wakili Vitalis alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusikilizwa(PH).

Hata hivyo, Wakili wa utetezi Elisalia Mosha uliiomba mahakama hiyo kumpa dhamana mteja wake kwa sababu mashtaka aliyonayo yanadhanika kisheria.

Hakimu shahidi alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya milioni 20, ambapo mshtakiwa alikidhi masharti hayo.

Hakimu Shahidi aliahirisha shauri hilo hadi Novemba 8,2017 kwaajili ya kusikilizwa

No comments:

Post a Comment

Pages