Mwenyekiti
wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Clement Sanga ameteua Kamati mpya ya
Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi.
Wajumbe
wanaounda Kamati hiyo ambayo ataiongoza yeye mwenyewe ni Shani Mligo (Makamu
Mwenyekiti), Boniface Wambura (Katibu), Issa Batenga, Leslie Liunda na Wakili
Saleh Njaa.
Wengine
ni Dr Ellyson Maeja, George Malawa, Isaac Chanji, Baruan Muhuza, Mbakileki
Mutahaba na Ally Mayay.
Kamati
hiyo ya TPLB ndiyo inayoshughulikia uendeshaji na usimamizi wa Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na Ligi Daraja la Pili (SDL).
Pia
Mwenyekiti ameteua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Uongozi ya TPLB.
Wajumbe hao ni Kanali Charles Mbuge ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Ruvu
Shooting, na Abuu Changawa (Majeki).
Kwa
mujibu wa Ibara ya 28(vi) ya Kanuni za Uendeshaji (Governing Regulations) za
TPLB, Mwenyekiti ana nafasi ya kuteua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya
Uongozi.
Boniface
Wambura
Ofisa
Mtendaji Mkuu
Bodi
ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
No comments:
Post a Comment