HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 21, 2017

BODI YA PAMBA TANZANZIA YATAKIWA KUONGEZA MBEGU MKOANI TABORA



NA TIGANYA VINCENT RS-TABORA

UONGOZI wa Bodi ya Pamba Tanzania umeomba kuongeza tani 148 ya mbegu za zao hilo baada ya wakazi wengi wa Mkoa wa Tabora kujitokeza kwa ajili ya kuoma zao hilo katika msimu wa mwa 2017/18.

Ombi hilo limetolea jana katika kijiji cha Mwanasimba Wilayani Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa uzinduzi wa msimu ujao wa kilimo cha pamba nchini.

Alisema kuwa baada ya zoezi la uhamasishaji wa kutoka katika vijiji mbalimbali katika Wilaya ya Igunga, Uyui, Urambo, Nzega na Kaliua watu wamehamasika na kujitokeza kulima zao hilo.

Mwanri alisema kuwa kabla ya zoezi la uhamasishaji kulikuwa na mahitaji ya tani 672.57 lakini baada kuendesha zoezi hilo idadi ya wanaohitaji mbegu imeongezeka na kufikia mahitaji ya tani 820.12 wakati hadi hivi sasa wamepokea tani 672.03.

Alisema kuwa Tabora ndio imechaguliwa kuwa mzalishaji wa mbegu za pamba na kitalu cha taifa kwa ajili ya maeneo mengine nchini na kwa hiyo haitakuwa vema kupanda aina nyingine ya mbegu zaidi ya UKM08.

Mwanri alitoa wito kwa uongozi kuhakikisha kuwa upungufu wa mbegu hizo unawafikia wakulima mapema kwa sababu zikishaanza kunyesha baadhi ya maeneo ni vigumu kufikika.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alitoa onyo kwa mkulima yoyote asidiriki kulima mbegu nyingine zaidi iliyopendekezwa na Bodi kwa ajili ya uzalishaji wa Mbegu na kuongeza kuwa kinyume cha hapo akikuta mkulima amepanda mbegu kinyume cha maelezo ya Serikali ataing’oa.

Kwa upande wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) Marco Mtunga alisema kuwa katika msimu ujao wa kilimo jumla ya tani 25,000 za mbegu zimetengwa kwa ajili ya wakulima ambapo 11,548 ni aina ya UKM08 na tani 13,452 ni UK91.

Alisema kuwa kwa upande wa Mkoa wa Tabora mbegu iliyosambazwa ni UKM08 na ndio pekee itakayolimwa kwa sababu ya kuwa kitalu cha Taifa kwa ajili ya kusambaza katika maeneo mengine katika Msimu wa 2018/19 ambapo maeneo yote yatalima aina hiyo mpya.

Mtunga aliongeza kuwa jumla ya ekari milioni moja na laki tatu zinatarajiwa kupandwa pamba msimu ujao wa kilimo katika mikoa 16 inayolima zao hilo hapa nchini.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo alisema kuwa tayari wameshapokea tani 500 za mbegu za pamba ambapo wameshazishambaza katika maeneo yote yanayolima zao hilo.

Alisema kuwa tayari viongozi mbalimbali wanaendelea kutoa elimu kwa wakulima ili waweze kuzalisha kulinga na sharia na kanuni za kilimo hicho kwa ajili ya kulinda heshima ya Wilaya ya Igunga kuwa kitalu cha Taifa.

No comments:

Post a Comment

Pages