Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli akishikana mkono na kupongezana na Mwenyeji wake Rais
wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi
wa Bomba la Mafuta ghafi litakalo toka Hoima nchini Uganda hadi eneo la Chongoleani
mkoani Tanga. Sherehe za uwekaji wa jiwe hilo zimefanyika katika eneo la
Mutukula Wilayani Kyotera nchini Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji
wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakisikiliza maelezo ya namna ya
bomba hilo la mafuta ghafi litakavyojengwa na kuanza kufanyakazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta
wakijadiliana jambo mara baada ya kupewa maelezo ya mradi huo mkubwa wa bomba
la mafuta ghafi.
Jiwe
hilo la Ufunguzi la Ujenzi wa Bomba hilo la Mafuta ghafi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji
wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakiondoka katika eneo la Mutukula
mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la bomba la mafuta.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasili
pamoja na Mke wa Rais wa Uganda Mama Janeth Museveni katika eneo la mpaka wa
Tanzania Mutukula kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha huduma za mpakani
kwa upande wa Tanzania na Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta
Museveni mara baada ya kuwasili upande wa Tanzania kabla ya ufunguzi wa Kituo
cha pamoja cha huduma za mpakani kwa upande wa Tanzania na Uganda.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais wa Uganda Mama Janeth Museveni wakiangalia ngoma katika
eneo la Mutukula upande wa Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakifurahia
ngoma za asili za watoto wa Uganda mara
baada ya kuwasili nchini humo huku Rais wa Uganda Yoweri Musevini akitazama
watoto hao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakifungua Ofisi za
Kituo cha pamoja cha huduma za mpakani kwa upande wa Tanzania. Wanne kutoka
kushoto ni Mke wa wa Rais Mama Janeth
Magufuli akishuhudia pamoja na Mke wa Rais Museveni Mama Janeth Museveni wa
kwanza kushoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Uganda Yoweri
Museveni wakizungumza na mamia ya wananchi hawaonekani pichani katika eneo la
Kyatera nchini Uganda mara baada ya ufunguzi wa Bomba la Mafuta. PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment