Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi
Angelina Madete, akizungumza wakati akiifungua warsha ya kimataifa ya
wanachama wa Umoja wa Posta Afrika kwa nchi zinazozungumza Kiingereza,
ilioanza jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Mount
Meru, Novemba 6 na kumalizika Novemba 10, 2017.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta duniani (UPU), Bi. Loilinda Dieme, akizungumza katika warsha hiyo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Bw. Younous Djibrine, akizungumza katika warsha hiyo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Bw. Deo Kwiyukwa akizungumza katika warsha hiyo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dkt. Haruni Kondo (kulia),
akiwa na Kaimu Postamasta Mkuu, Bw. Deo Kwiyukwa katika warsha hiyo.
Baadhi
ya sehemu ya washiriki wa warsha hiyo, kutoka Tanzania, wakiongozwa na
Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali za shirika, Bw. Macrice Mbodo (kushoto),
wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa.
Baadhi ya sehemu ya washiriki wa warsha hiyo, kutoka nchi mbalimbali, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa.
Baadhi ya sehemu ya washiriki wa warsha hiyo, kutoka nchi mbalimbali, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa.
Baadhi ya sehemu ya washiriki kutoka Tanzania, wakiwa katika mkutano huo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi
Angelina Madete (wa nne kulia, waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja
na washiriki wa warsha hiyo, mara baada ya kuufungua, jijini Arusha.
Kaimu
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Bw. Deo Kwiyukwa
akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kufunguliwa warsha
hiyo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dkt. Haruni Kondo
(katikati), akiwa na Kaimu Postamasta Mkuu, Bw. Deo Kwiyukwa (kushoto)
na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Bw. Younous Djibrine,
baada ya ufunguzi wa warsha hiyo.
Arusha-Tanzania
Arusha-Tanzania
WARSHA ya Kimataifa ya wanachama wa Umoja wa Posta Afrika kwa nchi zinazozungumza Kiingereza, imefanyika jijini Arusha, Tanzania ikizishirikisha nchi mbalimbali barani Afrika.
Katika warsha hiyo, ijulikanayo kama ‘operational readness for e-commerce,’ ilianza Novemba 6 na kumalizika Novemba 10, 2017, Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Angelina Madete, aliwataka kuwa na utayari wa kibishara ili waweze kuendana na mabadiliko ya tekinolojia.
"Tukiongeza
ubunifu wa kufanyakazi kwa mbinu za kisasa kwa kutumia huduma za
intaneti, wateja wengi watavutiwa na kuendelea kuwepo kwenye soko na
kuweza kukabiliana na ushindani wa kibishara." Alisema.
Naye
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Bw. Deo
Kwiyukwa, akizungumza katika warsha hiyo, alisema kwamba hivi karibuni
shirika lake limeanzisha Kampuni tanzu za uchukuzi na fedha kwa njia ya
posta, ambayo itakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi wengi hasa wa
maeneo ya vijijini lengo likiwa ni kukidhi mahitaji ya sasa na baadaye.
Warsha hiyo, imewashirikisha zaidi ya washiriki 50 kutoka nchi mbalimbali za Afrika, zinazozungumza lugha ya kiingereza, na imefadhiliwa kwa ushirikiano kati ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) na Umoja wa Posta Duniani (UPU).
Lengo la warsha hiyo ni kuziimarisha nchi wanachama kibiashara pamoja na kukamilisha mpango maalum wa taifa na kuweka malengo na kuanzisha mfuko maalum wa mradi wa huduma bora ‘quality of service fund (QSF) project’.
Pia kuweka mikakati maalum ya ushirikiano katika biashara ya mtandao e-commerce, kuweka viwango, kurahisisha na kuimarisha mifumo ya kiutendaji.
Warsha hii ni mwendelezo wa warsha nyingine iliyofanyika jijini Nairobi mwezi Mei 2017.
No comments:
Post a Comment