HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 12, 2017

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AREJEA NCHINI MARA BAADA YA KUMALIZA ZIARA YAKE NCHINI UGANDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye gwaride la Kimya lililoandaliwa kwa heshma na Jeshi la Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Uganda na kurejea nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakifurahia ngoma ya asili iliyokuwa ikipigwa na watoto wa nchini Uganda katika eneo la mpakani la Mutukula kabla ya kurejea nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa mpakani Mutukula upande wa Tanzania mara baada ya kuwasili akitokea Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi wa mpakani  Mutukula upande wa Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tau nchini Uganda. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Pages