Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka wakulima
kushirikiana na uongozi wa shule za msingi na sekondari Mkoani Rukwa kuanzisha
utaratibu wa kuwalisha wananfunzi wanapokuwa mashuleni.
Amesema kuwa anafahamu kwamba Mkoa wa Rukwa ni miongoni mwa
mikoa sita inayotegemewa kwa uzalishaji wa chakula nchini lakini haina
utaratibu wa kuwalisha wananfunzi wanapokuwa mashuleni jambo linaloshusha
ufaulu kwa wananfunzi hao.
“Tangu nimefika katika Mkoa huu wazee wananiambia hapa Rukwa
kuna chakula cha kutosha, utakula kuanzia asubuhi hadi kesho yake asubuhi,
namna chakula kilivyokuwa kingi lakini Je, humo mashuleni mwetu wanafunzi
wanapewa chakula?” Aliuliza.
Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na wazazi, walimu na
wanafunzi katika shule ya Msingi kipili kata ya kipili, Wilayani Nkasi katika ziara
yake ya kwanza tangu kuteuliwa na rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa
Mkoa huo na lengo ikiwa ni kutembelea na kukagua miradi mabalimbali ya wilaya
hiyo pamoja na kujitambulisha kwa wananchi.
Ameongeza kuwa wanafunzi wamekuwa wakitembea umbali mrefu
kwenda shule huku matumbo yakiwa matupu na hatimae wanashindwa kuelewa
wanachofundishwa darasani kwa kusikilizia njaa.
“Kuwa na chakula kingi haitakuwa na maana kama watoto wetu
wanashinda njaa mashuleni.”
No comments:
Post a Comment