Na
Beatrice Lyimo – MAELEZO - DODOMA
Serikali imesema
katika mwaka wa fedha 2017/2018 Jeshi la Polisi limetenga jumla ya
shilingi Bilion 2.2 kwa ajili ya
kupunguza madeni ya Wakandarasi waliotekeleza miradi mbalimbali ya Jeshi hilo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Mambo ya Ndani
ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni leo Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge
wa Baraza la Wawakilishi Jaku Ayoub
kuhusu madai ya Mkandarasi aliyejenga vituo vya Polisi Mkokotoni Unguja na
Madungu.
Mhandisi Masauni
ameeleza kuwa fedha hizo zilizotengwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa Kituo cha
Polisi Mkokotoni ambao umetengewa jumla ya shilingi Milioni 200 ikiwa ni sehemu anayodai
mkandarasi huyo.
“Serikali inatambua
madeni ya Wakandarasi wote ikiwemo Albatna Builing Contractor na ina nia ya
dhati ya kuyalipa madeni yote ya Wakandarasi na washauri elekezi waliohusika
katika miradi mbalimbali ikiwemo miradi iliyohusisha Jeshi la Polisi,”
amefafanua Mhandisi Masauni.
Wakati huohuo
Mhandisi Masauni amesema kuwa, Serikali imekuwa na mpango wa kupeleka fedha za
Maendeleo kwa ajili ya ukarabati na ununuzi wa samani katika Magereza nchini
ikiwemo Gereza la Karanga.
“Katika kukabiliana
na changamoto hiyo, Serikali inatekeleza mpango wa muda mrefu wa kuyaboresha
majengo hayo kwa kuyafanyia ukarabati mkubwa unaolenga kuyaimarisha,
kuyaboresha na kuyafanyia upanuzi,” amengeza Mhandisi Masauni.
Aidha amesema kuwa,
kutokana na ufinyu wa bajeti fedha hizo zimekuwa zikitolewa kwa awamu katika
Magereza mbalimbali nchini ili kufanikisha uboreshaji wa majengo hayo.
No comments:
Post a Comment