Kampuni ya Mtandao wa Simu za Mkoni wa TIGO imezindua huduma ya TIGO KOROSHO katika Mikoa ya Lindi na Mtwara kwa lengo la Kulipa wakulima wa zao la Korosho Mauzo yao Kupitia Tigo pesa kwa lengo la Kutatua kero ya za malipo kwa wakulima wa korosho ambao wanakabiliwa na Changamoto ya Upatikanaji wa Huduma za Kifedha hasa kwa wakulima wa Korosho walipo Maeneo ya Vijijini ambako hakuna taasisi za kifedha lakini Huduma ya Tigopesa inapatikana.
Huduma ya TIGO kOROSHO imeundwa ili Kumsaidia Mkulima aweze kupata Malipo kupitia Tigopesa kufika kwa wakati ,Usalama na Urahisi Tofauti na hapo awali ambapo Mkulima amekuwa akitumia muda mrefu kwenda katika taasisi za Kifedha na kukuta foleni ndefu ya kuchukua pesa.
TIGO KOROSHO pia Itamsaidia Mkulima kuwa na akiba ambayo ni salama na kumuongezea faida ya Gawio kutoka tigo pesa ambapo tayari kampuni ya TIGO inamawakala zaidi ya elfu3 katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akimsikiliza Meneja wa Tigo kanda ya Kusini {Lindi na Mtwara}Uthmaan Madati katika Uzinduzi wa Huduma ya TIGO KOROSHO ambapo Mkulima Atalipwa Malipo ya Korosho kupitia Huduma ya Tigo Pesa tayari Vyama 40 vya Msingi vya ushirika vimeingia Makubaliano Kutumia Huduma Hiyo katika Kurahisisha Kulipa wakulima wa Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa, akizungumza na Viongozi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo juu ya ulipaji wa wakulima kuhusiana na Huduma Ya Tigopesa katika uzinduzi wa huduma ya TIGO KOROSHO inayompa Fursa mkulima wa Korosho Kupokea malipo yake Kupitia Tigopesa kwa Wakulima wa Lindi na Mtwara.
Mkurugenzi wa tigo Kanda ya Pwani, George Lugata (wa katikakati), akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, juu ya huduma ya TIGO KOROShO inavyofanyakazi kwa wakulima wa zao la Korosho na jinsi ya kusambaza malipo kwa mkulima mmoja mmoja kwa kutumia Tigopesa na yayari wakulima wamekwishaanza kulipwa fedha zao za mnada wa kwanza.
No comments:
Post a Comment