Sehemu ya msaada wa vyakula mbalilmbali vilivyotolewa kama msaada na Kampuni ya QNET Tanzania kwa Kituo cha cha kulelea watoto yatima cha Khayraat Orphans Centre kilichopo Kigogo
Kati jijini Dar es Salaam.
Mahali kituo kilipo.
Mlezi wa Kituo
cha Kulelea Watoto Yatima cha Khayraat Orphans Centre kilichopo Kigogo
Kati, Bi. Khadija Hussein, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula kwa ajili ya sikukuu ya Krismasi na mwaka Mpya.
Mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki, akizungumza na waandishi wa habari.
Mwakilishi wa Kampuni ya QNET Tanzania, Benjamin Mariki, akionyesha mashine ya kusafisha maji ya kunywa kabla ya kuikabidhi kwa kituo cha kulelea Yatima cha Khayraat Orphans Centre.
Mwakilishi
wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki akikabidhi mashine ya kusafishia
maji ya kunywa (water purifier) kwa mlezi wa kituo cha kulelea
watoto yatima cha Khayraat Orphans Centre kilichopo Kigogo Kati, Bi.
Khadija Hussein.
Mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki, akikabidhi boksi la biskuti kwa mtoto, Asia Omary.
Mtoto Maulid Aboubakar akishukuru kwa niaba ya wenzake.
Mwakilishi
wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki akikabidhi mashine ya kusafishia
maji ya kunywa (water purifier) kwa mlezi wa kituo cha kulelea
watoto yatima cha Khayraat Orphans Centre kilichopo Kigogo Kati, Bi.
Khadija Hussein.
Mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki, akikabidhi boksi la biskuti kwa mtoto, Asia Omary.
Benjamin Mariki, akiagana na mtoto, Hussein Issa.
Mwakilishi
wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki akikabidhi vyakula kwa mlezi wa kituo
cha kulelea watoto yatima cha Khayraat Orphans Centre kilichopo Kigogo
Kati, Bi. Khadija Hussein.
Mwanaisha Ngubi akiagana na mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki.
Asia Omary akiagana na mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki.
Watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Khayraat Orphans Centrewakiwa katika picha ya pamoja.
Dar es Salaam, Tanzania
Moja kati ya taasisi
inayokua kwa kasi sana Tanzania ya masoko ya mtandao QNET, leo imetoa msaada wa
mashine yenye mfumo wa kusafisha maji ya Water purifier na chakula chenye
thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2 kwa kituo cha watoto yatima cha Khayraat jijini
Dar es Salaam.
Msaada wa QNET ni sehemu ya juhudi
za kampuni hiyo za kuwajibika katika jamii, ambazo zimeelekezwa katika kutoa
msaada wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa zaidi ya watoto 500 wenye
uhitaji katika kituo cha kulelea watoto yatima na kuwapatia chakula kwaajili ya
kuwawezesha kufurahia sikukuu za krimasi katika kipindi hiki cha sikukuu kama
watoto wengine.
Kwa mujibu wa mwakilishi wa
QNET Tanzania Benjamin Mariki, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja ina sera bora
ya uwajibikaji kwa jamii ambayo inatafuta kutoa kwa jamii inayoihudumia.
“Katika kampuni ya QNET,
tunaamini kuwa zaidi ya kusambaza bidhaa zenye ubora wa kiwango cha juu kwa
wateja wetu, tuna jukumu la kusaidia serikali na wadau wengine katika
kutekeleza shughuli ambazo zina athari nzuri kwa jamii, hasa miongoni mwa
wanajamii wenye uwezo mdogo,” alisema Mariki.
Mariki alisema kuwa msaada
uliotolewa kwaajili ya kituo ni pamoja na ufungaji wa mashine ya kusafishia
maji, kilo 100 za Mchele, kilo 100 za maharage, kilo 100 za unga, lita 60 za
mafuta ya kupikia, kilo 100 za sukari, kilo 100 za sabuni ya kufulia pamoja na
biskuti, pipi na juisi.
Akipokea msaada huo, Mwasisi wa
kituo cha Khayraat Orphans Centre, Bi Khadija Khussein aliishukuru kampuni ya
QNET kwa kutoa msaada akisema kuwa msaada huo utawasaidia kwa kiwango kikubwa
watoto walioko kituoni.
“Tunashukuru kwa msaada huo
tukiwa tunatambua kuwa mashine ya kusafishia maji ya water purifier itasaidia
katika kurahisisha upatikanaji wa maji safi na salama kwaajili ya watoto, hivyo
kutoa uhakika wa afya kwa watoto kwa kuzuia magonjwa yanayoambukizwa kwa maji kama
vile typhoid na Kipindupindu wakati vyakula vitawapa watoto nafasi ya kufurahia
sikukuu ya krimasi na mwaka mpya”. Alibainisha Bi Khussein.
No comments:
Post a Comment