Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akitaka ufafanuzi
kutoka kwa Mkurugenzi wa SUWASA Hamis Makala (Kulia) wa namna maji
machafu yanavyobadilishwa na kuwa safi ili kuendelea kutumika
alipofanya ziara katika Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira
Sumbawanga (SUWASA).
RUKWA, Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo ameiagiza Mamlaka ya
Maji safi na Usafi wa Mazingira Sumbawanga (SUWASA) kuwakatia maji wateja wenye
madeni sugu ili waweze kulipa madeni yao wanayodaiwa na taasisi mbalimbali za
serikali nchini.
Amesema kuwa uendeshaji wa Mamlaka hiyo utaendelea kuwa
mgumu endapo wataendelea kuwafumbia macho wateja wanaowadai na kushauri kuanza
kuangalia namna ya kutumia kadi za “pre- paid” (malipo ya kabla) katika huduma
hiyo ya maji ili kuzuia madeni yatokanayo na malipo baada ya matumizi.
“lazima muwabane walipe madeni, ni kama umeme kama mtu
halipi Kata, na huku kata maji, kama umewekwa utaratibu basi uheshiumiwe huo
utaratibu, nimesikia kwenye taafifa hapo kwamba kuna upungufu wa fedha
makudsanyo madogo na matumizi makubwa na wakati huo huo mna madeni makubwa na
watu hawalipi, kata,” Mh. Wangabo alisisitiza.
Ametoa kauli hiyo alipofanya ziara yake ya kwanza kwa Mamlaka
ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Sumbawanga (SUWASA) ili kujionea shughuli mbalimbali
zinazofanywa na mamlaka hiyo pamoja na kuufahamu kwa kina mradi wa Maji safi na
usafi wa mazingira katika miji saba nchini Sumbawanga ikiwemo, chini ya MDG–Initiative unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya pamoja na Serikali ya Ujerumani
wenye thamani ya Bilioni 31.
Aidha ameendelea kuwasisitiza Mamlaka hiyo kwa kushirikiana
na Manispaa pamoja na vyombo vya usalama kuhakikisha vyanzo vya maji
vinahifadhiwa na kupiga marufuku wale wote wanaofanya shughuli za kibinaadamu
katika vyanzo vya maji na kuwachukulia hatua wale wanaokiuka sheria hiyo ya
mazingira.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa SUWASA Hamis Makala amesema Mamlaka
hiyo inadai taasisi za kiserikali Shilingi Milion 69 na pia inadai watu binafsi
shilingi milioni 250 huku Mamlaka hiyo ikiwa inadaiwa shilingi milioni 100.6,
na kuongeza kuwa miongoni mwa changamoto wanazozipata ni kukauka kwa vyanzo vya
maji.
“Hadi Novemba mwaka 2017, SUWASA inadaiwa Milioni 100.6
kutoka kwa wadaiwa wake, mgawanyo wa madeni ni; Madawa ya Maji Shilingi Milioni
14.5, TRA Shilingi Milioni 13, EWURA Shilingi Milioni 6.8, Fidia Shilingi
Milioni 32, TANESCO Shilingi Milioni 17, Mita za Maji Shilingi milioni 6,
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Shilingi Milioni 11 kwaajili ya hati miliki,”
Makala alifafanua.
Halikadhalika Makala alisema kuwa deni hilo limekuwa kubwa
zaidi baada ya mkandarasi Herkin Builders kudai Shilingi Milioni 247.6 kama
riba ya kucheleweshewa malipo ya kujenga mradi wa dharura wa maji safi Sumbawanga
kati ya mwaka 2009 hadi March 2016.
IMETOLEWA NA
OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA
No comments:
Post a Comment