ZAIDI ya wanachama 500 wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita),
wanatarajiwa kushiriki mafunzo maalum ya kufungua msimu wa kilimo cha
Papai salama.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mkikita, Adam Ngamange jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Ngamange
alisema mafunzo hayo yatafanyika Februari 24 mwaka huu yatabeba ujumbe
'Papai salama open speech' kwa lengo la kuunganisha walaji, wazalishaji
na wataalam wa kilimo hicho.
Alisema
baada ya tafiti kufanyika wamegundua mkanganyiko mkubwa wa taarifa
hivyo kupitia mafunzo hayo ni wazi mabadiliko katika kilimo cha Papai
yatatokea.
"Tafiti
zinaonesha watalaam wanatofautiana kwenye idadi ya miche, uchimbaji wa
mashimo, umwagiliaji maji na utiaji mbolea hivyo mafunzo haya yataweka
washiriki kwenye mstari ili kukidhi ubora na ulinganifu wa soko la ndani
na nje," alisema.
Mkurugenzi
huyo alisema mafunzo hayo yatawakutanisha wabobezi na watendaji
mbalimbali katika kilimo hicho kipya cha Papai salama yatakuwa na awamu
tatu tofauti ili kujenga misingi imara katika kuleta unafuu wa
uzalishaji papai.
Alisema
Mkikita imejipanga kikamilifu katika kuhakikisha wakulima wa Tanzania
hasa wanaolima papai, mchaichai, mhogo na pilipili kichaa.
Aidha,
Ngamange alisema pamoja na mafunzo hayo wanatarajia kupokea ugeni
kutoka nchini Uturuki kutambua fursa za zao la papai nchini.
Pia
alisema wanachama wa Mkikita wanatarajia kufanya ziara ya mafunzo
Nchini Israel kuanzia Machi 11 mwaka huu na kugharimu dola za Marekani
2,000.
Halikadhalika
Mkikita imesaini makubaliano ya ushirikiano na Taasisi ya Hope For All
ambayo ina wanachama zaidi ya 5,000 ili waweze kushirikiana kwenye
nyanja za teknolojia na kilimo.
Akizungumzia
makubaliano hayo Mkurugenzi wa Hope For All Edgar Mwamfupe alisema
matarajio yao ni kuona mkulima anaheshima katika jamii.
Mwamfupe alisema kupitia Mkikita wanachama wao watafikia kwenye umilionea kwa kuwa kuna fursa za soko na biashara.
No comments:
Post a Comment