Mkuu
wa wilaya ya Kigamboni Mhe Hashim Mgandilwa,
amefanya ziara ya kutembelea mradi wa maji katika Kata ya Kisarawe II.
Akiwa
ameambatana na Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba,
wamepitia maeneo mbalimbali ambayo vituo vya kutolea maji vilipo na
kushuhudia baadhi vikitoa maji na baadhi vikiwa havitoi maji.
DC
Mgandilwa amemtaka mkandarasi anayejenga mradi huo kuhakikisha
anarekebisha maeneo ambayo yana itilafu ili maji yaweze kutoka katika
vituo vyote na kumaliza kero ya maji kwa wananchi wa mitaa husika.
DC
Mgandilwa ameongeza kuwa, Kama mkandarasi atashindwa kumalizia mradi
huo kwa wakati na kwa kiwango kinachostahili kwa kisingizio kuwa pesa
ilitumika yote wajiandae kuirudisha pesa hiyo haraka ili ifanye kazi
iliyokusudiwa kwani pesa iliyotolewa ilikuwa inatosha kabisa kumaliza
mradi huo vinginevyo watakuwa waliitumia vibaya.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa manispaa ya Kigamboni amesema kuwa mradi huo
aliupokea kutoka katika manispaa ya Temeke ukiwa katika hali ambayo sio
nzuri na umekuwa ukiendelea kusuasua licha ya kuufatilia mara kwa mara .
Ameongeza
kuwa kwa sasa anasubiria mkandarasi huyo amalizie mradi ukaguliwe ili
kujiridhisha na alete madai ya pesa ambayo atakuwa anadai alipwe kwani
serikali inataka wananchi wapate maji haraka.
No comments:
Post a Comment