Kaimu Postamasta Mkuu wa TPC, Hassan Mwang’ombe, akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Maria Sasabo (katikati), kuzungumza katika kuufunga mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Utumishi na Utawala kutoka wizarani, Kitolina Kippa.
Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Maria Sasabo akizungumza wakati akiufunga mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana. Wengine, kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa TPC, Hassan Mwang’ombe, kushoto ni Afisa Sheria Eunice Masigati na wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala Kitolina Kippa, wote kutoka wizarani.
Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Maria Sasabo akizungumza katika ufungaji huo. Kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu wa TPC, Hassan Mwang’ombe.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la wafanyakazi wa Shirika la Posta, wakifuatilia ufungwaji wa mkutano wao jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mkuu wa TEWUTA Taifa, Junus Ndaro, akitoa salamu za shukurani kwa Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Maria Sasabo, mara baada ya hotuba ya kuufunga mkutano huo.
Katibu Mkuu wa TEWUTA Taifa, Junus Ndaro, akitoa salamu za shukurani.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi, akifafanua jambo wakati wa ufungaji wa mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la wafanyakazi wa Shirika la Posta, wakiwa kwenye ufungaji wa mkutano huo.
Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Maria Sasabo (wa tano kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe (wa nne mwenye suti nyeusi), pamoja na wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa shirika hilo, mara baada ya kuufunga mkutano huo, jijini jana.
Katibu Mkuu (Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Maria Sasabo (wa tano kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe (wa tatu kushoto), pamoja na Kamati ya Utendaji ya Baraza Kuu la Wafanyakazi wa shirika la Posta.
No comments:
Post a Comment