HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 27, 2018

SPORTPESA KUKARABATI NYUMBA YA MADAKTARI ZANZIBAR


Picha ya pamoja kati ya (Baadhi ya wawakilishi/Uongozi wa SportPesa Tanzania) na uongozi wa Kizimkazi mkunguni mara baada ya kuzindua na kukabidhiwa mradi wa kujenga nyumba ya madaktari pichani, Kizimkazi Mkunguni, mkoa wa kusini, Zanzibar. Nyumba hizo zinatarajiwa kuchukua takribani miezi sita mpaka kukamilika na kukabidhiwa rasmi kwa uongozi wa Kizimkazi.

KAMPUNI ya Michezo ya Kubashiri nchini ya SportPesa Limited, imekubali kufanya ukarabati wa nyumba kwa ajili ya madaktari wawili wa Kituo cha Afya, Mkunguni eneo la Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja.Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi huo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti kutoka SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas amesema: 
“Ikiwa bado tuko mwanzoni mwa mwaka 2018, kampuni yetu tumeamua kutoa mchango wetu kwa jamii ya Zanzibar kwa kumalizia ujenzi wa nyumba ya madaktari ambayo ujenzi wa awali ulifanyika miaka 30 iliyopita, ujenzi mpya ni pamoja na kuongeza vyumba ili nyumba hiyo iweze kukaliwa na madaktari wengi zaidi.
Kwa Wanazanzibari wote, sisi kama SportPesa tupo kwa ajili yenu na si kwa upande wa Bara tu na ndiyo maana tumeamua kukarabati makazi ya madaktari kwani wapo kwa ajili ya kuokoa maisha yetu na ya watu wanaotuzunguka.Ujenzi wa nyumba hizi itaanza haraka iwezekanavyo na itachukua si zaidi ya kipindi cha miezi sita hadi kukamilika.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa nyumba hiyo, Diwani wa Wadiyamuyuni, Mustafa Mohammed Haji alianza kwa kuwakaribisha wawakilishi kutoka SportPesa kwenye wilaya yake na Zanzibar.

“Napenda kuipongeza kampuni yenu kwa kazi nzuri mnayoifanya ikiwa pamoja na mambo mbalimbali mnayofanya ili kuendeleza na kukuza sekta ya michezo nchini
Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Bwana Tarimba Abbas akiweka saini kwenye kitambu cha wageni kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kizimkazi, Mkunguni.

“Nilipopata taarifa juu ya ujio wenu kiukweli nilifarijika sana maana nawaamini na nategemea mambo mazuri kutoka kwenu kwani kwa maraya kwanza kusikia SportPesa ni kipindi kile mlivyoichukua timu yetu ya Jang’ombe kushiriki mashindano ya SportPesa Super Cup mwaka jana.”

Huu utakuwa ni muendelezo wa huduma za kijamii ambazo kampuni ya SportPesa imeendelea kuchangia ili kubadili maisha ya Watanzania katika Nyanja mbalimbali za kimaisha.

No comments:

Post a Comment

Pages