WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mwenyekiti wa Chama Cha
Walimu (CWT) mkoa wa Singida Mwalimu Aron Jumbe aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Akiwa hospitalini hapo leo (Jumamosi, Februari 10, 2018), Waziri Mkuu amefarijika baada ya kumkuta Mwenyekiti huyo na wagonjwa wengine waliolazwa kwenye taasisi hiyo wakihudumiwa vizuri.
Pia Waziri Mkuu amewajulia hali mabinti pacha walioungana Consolata na Maria Mwakikuti ambao nao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Waziri
Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wagonjwa hao na kuwaeleza kwamba
Serikali inadhamira ya dhati kuhakikisha inaboresha huduma za afya na
kwamba madaktari wataendelea kuwahudumia vizuri ili kuhakikishia afya
zao zinaimarika na kurejea katika shughuli zao za kila siku
Kwa upande wake,
Mwalimu Jumbe alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na kwenda
kumjulia hali. Aliwashukuru madaktari na wauguzi wa taasisi ya JKCI kwa
huduma nzuri wanazompatia tangu alipofika hospitalini hapo.
Kwa
upande wao Maria na Consolata walishukuru kwa msaada wa huduma za
matibabu wanazozipata na kwa sasa wanaendelea vizuri. Pia walimshukuru Waziri Mkuu kwa kwenda kuwajulia hali na kumtakia kheri katika shughuli zake
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, FEBRUARI 10, 2018.
No comments:
Post a Comment