HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 12, 2018

DK. MWAKYEMBE AFUNGUA MKUTANO WA 14 WA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI JIJINI ARUSHA.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) unaofanyika kwa siku tano jijini Arusha.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kinachotajwa kama Kikao kazi wakifuatilia kwa karibu Hotuba mbalimbali zilizotolewa wakati wa Ufunguzi wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari ,Sanaa,Utamaduni na Michezo ,Susan Mlawi akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali ,Dkt Hassan Abbas akizungumza katika mkutano hu unaofanyika katika Ukumbi wa mikuano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kinachotajwa kama Kikao kazi wakifuatilia kwa karibu Hotuba mbalimbali zilizotolewa wakati wa Ufunguzi wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Maofisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Pascal Shelutete, akitoa taarifa ya TAGCO kwa washiriki wa Mkutano huo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga, akifuatilia hotuba zilizotolewa wakati wa mkutano huo.
Mmoja wa Wadau  waliosaidia katika kufanikisha mkutano huo akipokea cheti kutoka kwa Waziri wa Habari, Sanaa,Utamaduni na Michezo, Dkt Harson Mwakyembe.
Washiriki wa Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi,Dkt Harson Mwakyembe, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini

WAZIRI wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe amewaagiza Maafisa Habari wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria,Kanuni na Taratibu za serikali huku akiwataka kuzingatia malengo ya kitaifa waliyojiwekea katika kikao kilichopita.

Mbali na agizo hilo Dkt Mwakyembe pia amesema serikali haita wavumilia maafisa habari ambao hawatambui wajibu wao  huku akiwafananisha na maafisa habari hewa  ambao wanageuza tovuti za Serikali kuwa magofu badala ya kuwa na habari mbalimbali zenye tija na maendeleo kwa taifa la Tanzania.

Dkt Mwakyembe ameyasema hay oleo wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano Serikali ,kinachofanyika katika Ukumbi wa mikutano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha kinachowakutanisha zaidi ya Maafisa Habari zaidi ya 300 kwa lengo la kuwajengea uwezo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Katika kikao hicho kinachoenda sambamba na Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO)kinafanyika wakati kukiwa bado kuna changamoto katika kada ya maafisa Habari wa taasisi za Umma ikiwemo uharaka wa ufikishaji wa taarifa za serikali kwa umma .

Katika mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali ,Dkt Hassan Abbas amewakumbusha washiriki wa mkutano huo kuenenda kimkakati huku akitoa nukuu za mcheza filamu Mashuhuri nchini Marekani ,Anord Schwazniger.
Naye Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ,Tanzania ,Alvaro Rodriguez amesema serikali ina umuhimu mkubwa wa kufundisha na kuhabarisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia zinazo iunganisha Dunia .

“Umoja wa Mataifa unaiona Tanzania ya leo na kesho yenye mafanikio mengi sana, Demkorasia, kufikia uchumi wa kati ,Elimu Bure,kupiga vita rushwa ni kati ya vitu vinavyoipa Tanzania sifa ya nchi iliyo tayari kuleta maendeleo ya nchi kwa ajili ya wananchi.”alisema Rodriguez.

Katika mkutano huo TAGCO ambacho ni chama kisicho cha kiserikali (NGO) kikiwa na madhumuni ya kukuza Mawasiliano na kuongeza Usambazaji wa  Taarifa ndani ya serikali na kati ya serikali na Wananchi  kimekabidh vyeti kwa Wadhamini wa mkutano huo ikiwemo Kampuni ya Clouds Media Group.

No comments:

Post a Comment

Pages