HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 23, 2018

Muhando, wenzake mguu sawa tamasha la Pasaka

.Wadau Dodoma kushuhudia uhondo April 8

NA MWANDISHI WETU

WARATIBU wa Tamasha la Pasaka ambalo hupambwa na nyimbo za injili za waimbaji wa kitaifa na kimataifa chini ya Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, wamesema maandalizi yote yamekamilika huku waimbaji wakiwa mguu sawa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msama Promotins, Alex Msama amesema waimbaji wote watakaoshiriki tukio hilo linalosubiriwa kwa hamu, kwa sasa wapo katika mazoezi ya nguvu.

Alisema ya kamba, awali tamasha hilo lilikuwa lifanyike katika mikoa miwili tu ya Mwanza hapo (Aprili Mosi) na Simiyu (Aprili 2), lakini sasa litafanyika pia mkoani Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri hapo Aprili 8.

“Tumeamua kuongeza kituo kingine cha tatu kwa ajili ya tamasha la Pasaka la mwaka huu, hivyo baada ya Mwanza na Simiyu, Aprili 8, uhondo utakuwa Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma,” alisema.

Hata hivyo, wakati Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ndiye atakuwa mgeni rasmi katika tukio la Mwanza litakalofanyika Uwanja wa CCM Kirumba,  mgeni katika Uwanja wa Jamhuri, atajulikana hivi karibuni.

Kuhusu mashambulizi ya uhondo wa nyimbo za Mungu katika Uwanja wa CCM Kirumba, Msama alisema waimbaji wanaanza maandalizi ya kuelekea katika jiji hilo kuwahi Aprili 1 kisha katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

“Mara zote baadhi ya waimbaji wamekuwa wakiimba live kwa kutumia vyombo jukwaani, hata safari hii itakuwa hivyo ili kuongeza mvuto zaidi kwa kila atakayefika uwanjani,” alisema Msama.

Kwa upande wa waimbaji, Msama alisema hadi sasa tayari waimbaji wengi wamekaa mkao wa utayari wakiongozwa na malkia wa Muziki wa injili nchini, Rose Muhando ambaye atatumia tamasha hili kuzindua albamu yake mpya ya ‘Usivunjike Moyo.’

Waimbaji wengine katika tukio hilo la kuutukuza ufalme wa Mungu, ni Angel Benard, Paul Clement, Christina Shusho, Beatrice Mwaipaja, Bonny Mwaitege, Ephraem Sekereti kutoka Zambia, Jesca Honole na wakali wengine.

Viingilio vya tukio hilo ni kwamba, katika Uwanja wa CCM Kirumba; wakubwa watalipa sh 5,000 huku watoto wakilipa 2,000 na mkoani Simiyu; wakubwa watalipa sh. 3,000 na watoto itakuwa shilingi 2,000.

No comments:

Post a Comment

Pages