WANAFUNZI 1622 wa Shule ya Msingi Uwondwe Shehia ya Mtambwe Mkoa wa
Kaskazini Pemba, wako hatarini kupata maradhi ya mripuko iwapo hatua za haraka
hazitachukuliwa kutokana na kujisaidia Vichakani karibu na eneo la shule
kufuatia upungufu wa vyoo.
Taarifa hiyo ilitolewa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Khadija
Said Khalfan mbele ya mkuu wa Mkoa huo alipofanya ziara ya khafla kujione
mwenyewee tatizo hilo.
“Mh; kiukweli shule yetu
ina vyoo vitatu na idadi ya wanafunzi kama hivyo na kipindi hichi mvua ndio
tukasema kuwa tumo katika hatari ya maradhi mengi ikiwemo ya mripuko kama hatua
za haraka hazikuchukuliwa” alieleza Mwalimu Mkuu.
Alifahamisha kuwa watoto wengi wanao tumia shule hiyo ni wadogo
ambao wanaposhikwa na haja kubwa na ndogo hukimbilia vichaka ili kuondoa shida yao
kutokana hivyo vyo kuwa vibovu ambavyo alieleza kuwa vimejengwa tangu kabla ya
Mapinduzi.
Naye Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman
ambaye ameeleza kusikitikishwa na hali hiyo na kuitaka Serikali ya shehiya hiyo
kuhakikisha shule hiyo inapata vyoo haraka.
Alieleza kuwa kukosekana kwa vyoo katika shule inapelekea hata
maendeleo ya shule kuwa mabovu kwani mara nyingi watoto huwa nje ya eneo la
shule.
Alisema huo ni uharibifu wa Mazingira ambao haukubaliki na
unatakiwa kuchukuliwa hatua ya haraka ili kuhami Maisha yao.
Aidha Mkuu wa Mkoa ameahidi kuzungumza na wananchi wenye asili
ya Mtambwe kuwashawishi kusaidia maendeleo ya shule hiyo .
Shule ya Uwonde imejengwa mwaka 1934 , inakabiliwa na changamoto
ya vyoo pamoja na upungufu wa walimu
ambapo kwa sasa inajumla ya walimu 19 na vyumba vya madarasa 22.
No comments:
Post a Comment