NA SULEIMAN MSUYA
KAMPUNI
ya Simu ya Tigo Tanzania na Kampuni ya Kiteknolojia Uber zimeingia
makubaliano ambayo yatasaidia watumiaji wa usafiri Uber kupata usafiri
huo bila kuwa kifurushi cha mtandao maarufu (bado).
Wakizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakurugenzi wa kampuni
hizo waliweka bayana kuwa makubaliono hayo yana faida kwa pande zote
mbili.
Mkurugenzi wa Tigo
Tanzania, Simon Karikari alisema kampuni yao ni moja ya kampuni yenye
nembo kubwa nchini hivyo ubia huo walioingia na Uber utazidi kupanua
wigo wao wa kibiashara.
Karikari
alisema wateja wa tigo watapata huduma hiyo bila ya kuwa na kifurushi
cha mtandao jambo ambalo litaongeza wateja wa usafiri wa Uber.
"Uber
ni kampuni ya Kimataifa hivyo ubia huu ni ishara tosha kuwa Tigo
inakubalika na sisi hatutawaangusha kwani tumeshika asilimia kubwa ya
soko la biashara ya mawasiliano ya simu nchini," alisema.
Alisema
kwa sasa Tigo ina zaidi ya wateja milioni 11.3 hivyo ni matumaini yao
kuwa ubia huo na Uber utachochea ongezeko kubwa la wateja kwa muda mfupi
na pande zote kunufaika.
Kwa
upande wake Meneja Mkazi wa Uber Tanzania, Alfred Msemo alisema ubia
huo ni muhimu kwao na wateja wao kwa kuwa watapatikana bila gharama.
Msemo
alisema madereva na wateja ambao wanatumia mtandao wa Tigo watakuwa
wanawasiliana popote bila gharama jambo ambalo awali iilikuwa
changamoto.
Alisema
usafiri wa Uber umefanikiwa kutoa ajira zaidi ya 3000 na kuhudumia watu
zaidi ya 200,000 kwa mwezi hivyo ubia huo utaongeza watumiaji wengi.
Meneja
huyo alisema mikakati yao ni kuhakikisha kila mkazi wa jiji la Dar es
Salaam anaweka kipaumbele katika kutumia Uber kama njia ya usafiri wa
haraka kufika anapotaka.
"Tumekuwepo
Tanzania takribani miaka miwili sasa kwa mafanikio makubwa lakini hatua
ya leo kuingia ubia na Tigo ni hatua kubwa zaidi kibiashara naamini
wateja wataongezeka maradufu," alisema.
Msemo alisema matarajio yao ni kuhakikisha wanafukia mikoa mingine kwa siku za karibuni ili kusambaza huduma hiyo.
Alisema kwa miaka miwili huduma ya Uber Tanzania imefanikiwa kuhudumia wageni kutoka nchi 70 duniani ambao wa wana App yao.
No comments:
Post a Comment