Makamu mwenyekiti wa kamati ya michezo ya mei mosi kitaifa Joyce Benjamini akitoa kero ya kamati ya mashindano ya mei ya mosi taifa inasikitishwa na kupungua kwa timu shiriki katika mashindano hayo yanaendelea mkoa wa Iringa kutoka timu kumi na Tano (15) mwaka jana hadi timu kumi (10) mwaka huu 2018 mbele ya katibu tawala msaidizi mkoa Majuto Njanga aliyekuja kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza.
Viongozi mbalimbali wa michezo ya mei mosi wakiwa jukwani wakipokea maandamano ya timu shiriki zilizokuwa zikiingia uwanjani.
Baadhi ya viongozi na wadau wakiwa jukwaani wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mei mosi katika uwanja wa kumbukumbu ya Samora.
Na Fredy Mgunda, IRINGA
KAMATI ya Mashindano ya Mei ya Mosi Taifa inasikitishwa na kupungua kwa timu shiriki katika mashindano hayo yanaendelea
mkoa wa Iringa kutoka timu kumi na Tano (15) mwaka jana hadi timu kumi (10)
mwaka huu 2018.
Kauli hiyo imetolewa na makamu
mwenyekiti wa kamati ya michezo ya mei mosi kitaifa Joyce Benjamini wakati wa
uzinduzi wa michezo ya mei mosi kwenye kiwanja cha kumbuku ya Samora Mkoani
Iringa.
Benjamini alisema kuwa kupungua kwa idadi
ya timu shiriki kunatokana na baadhi ya mashirika ya sekta ya UMMA na serikali
kushindwa kupeleka timu kwa visingizio vya ukata ili hali timu ya Rais ikiwa
imeshiriki mashindaano hayo.
“Mheshimiwa mkuu wa mkoa tunapenda
kutoa malalamiko yetu juu ya kupungua kwa hizi timu na kusingizia ukata wa pesa
jambo ambalo sio kweli kwa kuwa waziri mkuu,makamu wa rais na rais wetu ni viongozi
wapenda michezo hivyo uoga wao ndio umefanya kushindwa kuzileta timu zao
zishiriki mashindano haya” alisema Benjamini
Benjamini alisema kuwa hakuna mahali
ambako rais amekataza wafanyakazi wa serikalini kutoshiriki michezo
mbalimbali,viongozi wetu wa serikali wamekuwa waoga kwenye matumizi ya fedha za
serikali,anachokitaka Rais ni uhalisia wa matumizi ya fedha katika maeneo
husika.
“Mhesmimwa mkuu wa mkoa hata
ukiangalia kwenye ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi mwaka 20102
ibara ya 61 ukurasa wa 218 hadi 219 unasema wajuu ya kuinua na kuendeleza
michezo hapa nchini,sasa kwanini viongozi hawafuati ilani hiyo” alisema Benjamini
Benjamini alizitaja timu
zinazoshiriki mashindano hayo mkoani Iringa kuwa ni timu kutoka Ofisi ya Rais
–Ikulu,Wizara ya Uchukuzi,Chuo Kikuu kishiriki cha Afya na sayansi
(MUHAS),Hifadhi za Ngorongoro,Geita gold mine (GGM),Mamlaka ya mapato Tanzania
(TRA),Shirika la umeme Tanzania (TANESCO),Tumbaku-TTPL ya Morogoro,Ukaguzi na
Wenyeji timu ya RAS Iringa.
“Hizo ndio timu zilifika kwenye kituo
hiki mkuu lakini nichukue nafasi kuzitaja timu ambazo zimenipa simanzi ya
kutoshiki mashindano haya ni kama vile timu ya Ofisi ya Waziri mkuu,Wizara ya
Mambo ya Ndani,Maliasilina Utalii,Wizara ya afya maendeleo ya jamii,timu za
mashirika ya UMMa kama TTCL,Posta,Bima,NSSE na nyingine nyingi ambazo zilikuwa
washirika wazuri wa michezo ya mei mosi” alisema
Akizungumza kwa niamba ya mkuu
wa mkoa wa Iringa Amina Masenza, katibu tawala msaidizi mkoa Majuto Njanga amezionya
timu ambazo zinashiriki kwenye michuano ya mei mosi kuacha kuchukua wachezaji
ambao sio wafanyakazi kwani kufanya hivyo kunapunguza ladha ya mashindano
hayo.
Njanga alisema kuwa michezo
hujenga undugu na furaha baina ya wanamichezo hivyo kuwaingiza wachezaji ambao
sio wafanyakazi kwenye mashindano hayo wataondoa maana halisi ya mashindano
hayo jambo ambalo linaweza kuwafanya kushindwa kufikia malengo yao
waliojiwekea.
“Mashindano haya ni ya
wanamichezo wafanyakazi,kuna wale wanamichezo ambao sio wafanyakazi ambao
wanajulikana kama mamluki au wavamizi kwamba hapa sio mahala pao nawasihi
tuchezeshe wafanyakazi halisi ili mshindi apatikane kihalali na sio vyenginevyo
kwa sababu ni hatari sana kumleta mwanamichezo ambaye sio mfanyakazi kwenye
michezo hii anaweza kuvunjika mguu au akifa kwa mfano hatuombei itokee hiyo
itakuwaje “Alisema Njanga
Aidha Njanga alizitaka
timu hizo kuacha kuwatumia wachezaji wa aina hiyo kwani wana madhara makubwa
hasa pale yanapokuwa yakijitokeza kwa kuzitaka timu zenye utamaduni huo
kuhakikisha wanaondokana nao.
Hata hivyo Njanga alionekana
kukerekwa na baadhi ya menejimenti za Taasisi,Mashirika na makampuni mbalimbali
kuwa na utashi wa kutokupenda michezo na wengine kwa kisingizio cha ukosefu wa
fedha kuacha kufanya hivyo badala yake wamuunge mkono Rais Jakaya Kikwete
katika jitihada zake za kuinua na kuendeleza michezo hapa nchini.
Akizungumzia waamuzi
wanaochezesha mashindano hayo, Njanga aliwataka kuchezesha kwa haki bila
upendeleo kwa kufuata sheria za mchezo husika ili mshindi aweze kupatikana
kihalali kwa sababu wakienda kunyume chake wanaweza kusababisha tafrani na
manung’uniko kwa baadhi ya timu shiriki.
Hali kadhalika aliwataka
kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu wakati wote wa mashindano
ikiwemo kukubaliana na matokeo pindi watakapojikuta wamefungwa wakati wa
mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment