HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 20, 2018

MRADI WA UTOAJI HUDUMA ZA JAMII KWA UMMA WAZINDULIWA ZANZIBAR

Na Mauwa Muhammed, Zanzibar

Taasisi zisizo za kiserikali zimezindua mradi wa uwajibikaji katika jukumu la utoaji wa  huduma za jamii kwa umma zinazotekeleza mamlaka ya maendeleo ya serikali za mitaa.

Akizindua mradi huo wa kuinua uwajibikaji katika utoaji wa huduma Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Mzuri Issa, huko katika ofisi yao iliyopo Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.

Amesema mradi huo unahitaji mashirikiano ya pamoja na mamlaka ya Halmashauri na ofisi za Wilaya ambazo ndizo zinazosimamia utoaji wa huduma kwa jamii kupitia utaratibu mpya wa ugatuzi wa madaraka.

Amesema miongozi mwa mambo yanayohimizwa katika kutekeleza mradi huo ni kuimarisha mifumo ya kitasisi na sheria ili kuirahisishia ushirikishwaji imara kwa wananchi kuanzia upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo katika maeneo yao.

Mradi huo unashirikisha wilaya sita za Zanzibar, unatekelezwa na TAMWA kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wandishi wa habari za maendeleo  Zanzibar (Wahamaza) na jumuiya ya uhifadhi wa mazingira pemba (Ngeraneko). 

Wilaya wenyewe ni Kaskazini A,Kati,Kusini kwa Kisiwa cha Unguja Ungja na Wete,Chake Chake na Micheweni kwa Wilaya za Pemba ambapo mradi huo utachukua miezi kuminatano.

Bi Asha Aboud Muwasilishaji wa ripoti ya utafiti waliofanya wa uwiyano wa sheria ya serikali za mitaa Zanzibar na sera za utawala bora kumebainika kuwepo na kasoro katika suala la ushirikishwaji wananchi katika mipango inayohusu maendeleo yao.

Alisema moja ya msingi wa utawala bora ni ushirikishwaji wa wananchi wawe pamoja katika kutoa mamuzi na pia wawe pamoja katika mapato na matumizi.

Ni vyema kuona wananchi wana sehemu katika halamshauri wanatakiwa kushiriki na kutelekezamikataba ya kimataifa kuwepo (Gender Equality).

Kuangalia uwajibikaji wa viongozi na ufikiaji wa rasilimali na kuangalia miradi ya maendeleo katika jamii

Amesma lengo la ripoti hiyo ni kuangalia upatikanaji na ufikiaji wa huduma za kijamii kama kuwepo shule na hospitali ambazo zinaruhusu makundi yote ya kijamii yanafaidika hasa walemavu kuwepo miundombinu ya walemavu.

Pia ripoti hiyo imeangalia ushiriki wa wanachi wakiwemo makundi malum katika mipango ya maendeleo pia ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wa mipango ya bajet.

Pia  ripoti hiyo imeangalia huduma muhimu kwa wananchi zinapatuikanaje na pia wananchi wanaridhika nazo na ikiwa hawaridhiki nazo malalamiko yao wanayafikisha wapi.


 Ametoa wito kwa malaka zinazohusia kutekeleza sheria mpya ya upelekaji madaraaka ya kutoa majukumu ya utoaji huduma kutoka serikali kuu kupeleka mikoani.

Amesema ni vyema kutambua umuhimu wa kushirikishwa katikamasuala ya upangaji wa bajet  na utekelezaji wake.

Akichangia katika mjadala wa ripoti hiyo mjumbe kutoka Wilaya ya Kusini Halida Nassor alisema Halmashuri hazina uwazi kuhusu  mfuko wa Jimbo kwani hawajui unatumika vipi.

Alisema kumekosekana umoja ndani ya jamii na ndio mana taratibu haziendi sawa.

Nae mshiriki Ali Hamadi Afisa kutoka wilaya ya kati Unguja alisema wananchi wanakosa muda wa kushirikishwa kutokana na kuwepo njia isiyo sahihi ya kuwafikia  ambapo hupelekea kuwepo ushirikishwaji mdogo kwa jamii.

Alisema ni vyema kutumia njia iliyo  muafaka ili  kuwafikia wananchi wa makundi yote  bila kujali jinsia.  

Nae kwa upande wake Zawadi Pandu Vuai Diwani wa wadi ya makunduchi amesema sehemu nyingi wananchi wamekuwa haawashirikihwi katika mipango ya maendeleo yao .

Alisema ni vyema kuwepo mipango  ili wanawake waweze kuingia katika nafasi za  kamati katika Majimbo

Kwa upande wake mshiriki  Wahida Kondo alisema  katika Idara ya Utawala Bora kumekuwepo Program tofauti kupitia vyombo vya habari za kuwaelimisha  wananchi .

Alisema kuna badhi ya maeno wanawake wamekuwa wanashindwa kujitokezakutokana na kukoza elimu ya kujua umuhimu wa wajibu wao na wengine kukumbwa na majukumu ya kifamilia.

 Hivyo aliwataka wanawake  kubadilika ili kuwendana na wakati wa sasa ili kuzitambua haki zao.
 

No comments:

Post a Comment

Pages