Timu ya Taifa ya Vijana U20 (Ngorongoro Heroes) imerejea
nchini Leo ikitokea nchini DR Congo kwenye mchezo wake wa marudiano wa kufuzu
fainali za Africa za Vijana U20 dhidi ya DR Congo.
Wachezaji wa Ngorongoro ambao wamefanikiwa kuivusha timu
hiyo kwenda raundi ya pili wamepewa mapumziko ya siku tatu kwa mujibu wa program
ya Kocha Mkuu Ammy Ninje.
Katika raundi ya pili Ngorongoro Heroes watacheza dhidi ya
Mali mwezi ujao mchezo wa kwanza wakianzia nyumbani.
SERENGETI
BOYS KUPIGA NUSU FAINALI KESHO
TIMU YA Taifa ya Vijana U17 (Serengeti Boys) kesho inatupa
karata yake muhimu kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Kenya.
Mchezo huo utachezwa saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Muyinga
nchini Burundi.
Kufuzu hatua ya nusu fainali Serengeti Boys walitoka sare
ya bao 1-1 dhidi ya Uganda kwenye mchezo wa kwanza kabla ya kuifunga Sudan kwa
magoli 6-0 kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B.
Tunaitakia kila la kheri Serengeti Boys iweze kufanya
vizuri kwenye mchezo huo wa nusu fainali.
Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Serengeti Boys.
MECHI
YA SIMBA NA YANGA MAGETI KUFUNGULIWA MAPEMA,JESHI LA POLISI LAWEKA ULINZI MKALI
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
utakaowakutanisha Simba na Yanga Jumapili Aprili 29,2018 uliopangwa kuchezwa
saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa Tiketi zinaendelea kuuzwa kupitia Selcom.
Yeyote anayetaka kununua tiketi hizo kupitia Selcom
anachotakiwa kufanya ni kujaza pesa kwenye kadi yake ya Selcom ambayo
inamuwezesha kuweza kununua tiketi hizo kupitia simu ya mkononi.
Mageti yanatarajia kufunguliwa mapema kuanzia saa 2
asubuhi ambapo vyakula na vinywaji vitapatikana ndani.
Jeshi la Polisi limehakikisha ulinzi utakua wa hali ya juu
na kuwatahadharisha wale wote wenye nia ya kufanya vitendo vya uovu.
Mamlaka ya Uwanja imethibitisha kuongezeka kwa camera za
Uwanjani ambapo sasa zimefikia 109 ambazo zitakuwa zinafuatilia matukio yote
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TF
No comments:
Post a Comment