WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea katika Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma.
Ameyasema
hayo leo (Jumanne, Aprili 24, 2018) mara baada ya kukagua maandalizi
hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma, ambapo
amesema maandalizi yanaendelea vizuri.
Waziri
Mkuu amejionea maonesho mbalimbali yakiwemo ya kikundi cha halaiki
ambacho kinaundwa na wanafunzi 2,000 kutoka Manispaa ya Dodoma pamoja na
maonyesho ya kujihami na maadui yaliyooneshwa na Jeshi la Magereza.
“Nimeridhika
na kazi ambayo mmeifanya, nawaruhusu muendelee kushirikiana katika
kukamilisha maeneo ambayo yamesalia na kuanzia kesho tujiandae kuwapokea
wageni kutoka maeneo mbalimbali.”
Alhamisi
Aprili 26, 2018 Watanzania wanatarajia kuadhimisha miaka 54 ya Muungano
tangu Tanganyika ilipoungana na Zanzibar, chini ya waasisi wake Hayati
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
JUMANNE, APRILI 24, 2018.
No comments:
Post a Comment