SPIKA
wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Dk. Martin Ngoga ameishukuru na
kuipongeza Serikari ya Tanzania kwa ujenzi wa miradi mbalimbali ya
maendeleo ukiwemo wa reli kwa sababu inaleta manufaa hata kwa nchi
jirani.
"Miradi
hiyo ambayo kwa sasa inatekelezwa kwa kasi si kwamba inachochea ukuaji
wa uchumi wa Tanzania, bali hata wa nchi nyingi za jirani kwa kuwa nazo
zitanufaika na miradi hiyo kwani si nchi zote zina bandari".
Dk.
Ngoga ameyasema hayo leo (Jumatatu, Aprili 23, 2018) alipokutana na
kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Bungeni mjini
Dodoma.
Amesema
tayari wamejadili ripoti iliyotokana na ziara iliyofanywa na wabunge
hao katika upande wa korido ya kuishi na korido ya kaskazini ambapo
wametoa mapendekezo yatakayofanyiwa kazi na baraza la mawaziri.
"Tayari
tumeshajadili miswada miwili inayohusu Itifaki ya Sarafu Moja ambayo ni
mswada wa taasisi ya Fedha na mswada wa Takwimu yote ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki ya mwaka 2017."
Pia
Spika huyo amesema wamefurahia uwepo wao nchini, ambapo mbali na
shughuli zao za kibunge pia kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma wameshiriki kampeni ya kukijanisha Dodoma kwa kupanda miti 1,000 kwenye eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Kwa upande wake,
Waziri Mkuu amesema amefarijika na uamuzi wa Bunge la EALA kufanya
vikao vyake katika nchi wanachama kwa sababu unatoa fursa ya kujua
mazingira ya nchi hizo pamoja na maendeleo yake.
Amesema
nchi wanachama wanamatumaini makubwa na bunge hilo katika kuimarisha na
kuboresha maendeleo ya mataifa yao, hivyo amewatakia mjadala mwema.
Katika hata nyingine,
Waziri Mkuu amewakaribisha wabunge hao na marafiki zao kuja kuwekeza
kwenye sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya viwanja, utalii, kilimo na
madini.
Kwa
mara ya kwanza vikao vya Bunge la Afrika Mashariki, (EALA) vinafanyika
Dodoma katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa ulipo ndani ya Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania. Vikao hivyo vilianza Aprili 17, 2018 na
vinatarajiwa kumalizika Aprili 29, 2018.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
JUMATATU, APRILI 23, 2018.
No comments:
Post a Comment