WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwaleo (Jumatano, Aprili, 25, 2018) ameshiriki maziko
ya aliyekuwa mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu marehemu Bw. Atufigwege
Mwakasege yaliyofanyika katika makaburi ya Kikuyu mjini Dodoma.
Bw.
Mwakasege ambaye alihamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Februari 29, 2016
akitokea Ofisi ya Rais-TAMISEMI amefariki dunia Aprili 23 mwaka huu
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa baada ya
kuugua.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi
Jenista Mhagama amesema kifo hicho kimeiachia pengo kubwa kwa Ofisi ya
Waziri Mkuu pamoja na familia.
“Natumia
fursa hii kutoa pole kwa wanafamilia hususan mjane na watoto. Marehemu
ameacha pengo ndani ya familia, hivyo tumuombe Mwenyezi Mungu awape
uwezo na nguvu ya kuweza kuhimili pengo hilo.”
Marehemu
Bw. Mwakasege ambaye alizaliwa Desemba 25, 1959 katika kitongoji cha
Mwanjelwa mkoani Mbeya, ameacha mjane Bibi Judith Mwakasege pamoja na
watoto wane ambao ni Henry, Joel, Eva na Kelvin Mwakasege.
Maziko
hayo pia yamehudhuriwa na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mama Mary
Majaliwa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa
Faustine Kamuzola, Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna
Tarishi, Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
JUMANNE, APRILI 25, 2018.
No comments:
Post a Comment