HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 09, 2018

WATU NANE WA FAMILIA MOJA WAFA AJALINI MBEYA

Noah yenye namba za usajili T 649 DEA na Basi aina ya Scania kampuni ya Igembesabo yenye namba za usajili T 672 CLR na kusabisha vifo vya watu nane wa familia moja katika Eneo la Igodima kata ya Mwansekwa nje kidogo mwa jiji la Mbeya katika barabara ya Mbeya Tabora. (Picha na Kenneth Ngelesi).

NA KENNETH NGELESI, MBEYA

WATU nane wa familia moja wamefariki dunia papo hapo na mmoja kujehuriwa baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kutoka wilayani Chunya kwenda Mbeya Mjini, kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Igembesabo katika eneo la Igodima barabara kuu ya Mbeya- Tabora nje kidogo ya ya jiji la Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Mussa Tahib, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 5:00 asubuhi katika eneo hilo Igodima Kata ya Mwasekwa ikiwa ni umbali wa kilomita tano kutoka katikati ya jiji la Mbeya na kwamba marehemu hao walikuwa wanawahi mazishi ya ndugu yao jijini Mbeya.

Kaima kamanda Tahib alisema wanafamilia hao walikuwa tisa na mmoja kati yao alisalimika japo alijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Mbeya kwaajili ya matibabu na kwamba hakuna majeruhi wala kifo chochote kwenye basi.

Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Noah yenye namba za usajili T 649 DEA na Basi kubwa aina ya Scania kampuni ya Igembesabo yenye namba za usajili T.672 CLR linalofanya safari zake Mbeya- Chunya katika kijiji cha Isanganawna na wakti huo lilikuwa litokea Mbeya Mjini kuelekea Wilayani Chunya.

Akizungumzia Chanjo cha ajali Kaima kamanda Tahib alisema ni kutokana na uzembe wa madereva wote wawili kwani dereva wa basi alikuwa anaendesha gari upande ‘Site’wa kulia ambao ni kwa ajili ya magari yanayotokea Chunya huku Dereva wa Noah akiendesha gari kwa mwendo kasi.

“Ajali nii ni uzembe wa madereva wote wawili wawili lakini kinachoumizaa zaidi hawa ndugu walikuwa wanaenda kuhudhuria mazishi ya ndugu yao lakini sasa wanafamilia wamepata msiba mkubwa zaidi kwa sababu ya uzembe” alisema Tahib

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William Ntinika,suaa la kusitoshwa sana kwani na kwamba ni msiba mkubwa, huku akieleza kuwa ajali hiyo ni ya tatu ndani ya siku tano ndani ya wilaya yake hivyo ameviagiza Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Wilaya hiyo kuimarisha doria kwenye maeneo yote korofi ambayo ajali zimekuwa zikitokea mara kwa mara.

Aidha katika hatua nyingine Ntinika aliwata madereva na watumiaji wote wa barabara kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali za kizembe kama hizo ambazo zingeepukika huku akiviagiza vyombo vya dola kuwachukulia hatua za kisheria madereva wote wanaokiuka Sheria za Usalama barabarani ili kuhakikisha ajali hizo zinapungua.

“Eneo hili kuna ajali ilitokea juzi na kujehuri watu 44 baadhi ya majeruhi bado wapo hospitalini lakini pia jana (juzi), pale mlima nyoka barabara ya Mbeya Njombe ilitokea ajali nyingine na kuua wawili hivyo lazima vyombe vyetu vifanye kazi saa 24 kwenye maeneo haya korofi,” alisema Ntinika.

Naye Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) Mkoa wa Mbeya, Denis Daud, alisema gari ndogo aina ya Noah iliyokuwa imebeba wanafamilia hao, haijasajiliwa kubeba abiria.

Hata hivyo alisema magari yote yaliyosajiliwa kufanya kazi kati ya Jiji la Mbeya na Chunya yako imara na kwamba ajali zinazotokea ni kwa sababu ya uzembe wa madereva.

Alisema magari hayo kabla ya kusajiliwa kuanza kufanya kazi katika barabara hiyo ni lazima yakaguliwe na mkaguzi wa magari ili kujiridhisha na mifumo yake.

Ajali hiyo niya pili kutokea katika eneo hilo ikiwa ni siku tano zimepita tangu basi aina Fuso lililokuwa likitokea Chunya kuja Mbeya mjini kuacha njia na kupinduka na kusababisha watu 44 kujehuriwa katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages