HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 27, 2018

FINCA yazindua shindano maalum

 Ofisa Mkuu wa Biashara wa Finca Microfinance Bank, Emmanuel Mongella, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa programu ya ya miezi mitatu na shindano la kuwaongezea uwezo wajasiriamali wadogo kwa kuwapatia stadi za biashara. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Finca Microfinance Bank, Nicholous John. (Picha na Francis Dande).
 Waandishi wa habari wakichukua matukio.
 Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Finca Microfinance Bank, Nicholous John.

NA MWANDISHI WETU

BENKI ya FINCA Microfinance imetangaza uzinduzi wa programu ya miezi mitatu na shindano ambalo linalengo la kuwaongezea uwezo wajasiriamali wadogo kwa kuwapatia stadi za biashara, ufahamu na kisha kuwapatia zaidi ya fedha taslim sh Millioni 10 kwa wazo bora la biashara litakalokuwa limewasilishwa. 

Shindano hilo linalojulikana kama 'Kuza Ofisi na FINCA’ kwa kuanzia litafanyika katika wilaya nne za Mkoa wa Dar es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo.  Wilaya hizi zitaambatanishwa katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege.

Akizungumza wakati wa uzinduzi jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John, alisema kwamba lengo ni kuwapatia elimu ya biashara na fedha wamiliki wa biashara ndogo ndogo ambao baadae itapelekea katika kukuza biashara zao,  Mshindi wa programu na shindano hili atawezeshwa kifedha kuendeleza biashara zake ndogo ndogo ziliyopo.

"Shindano hili litashirikisha wateja wa FINCA wenye akaunti na wale ambao wanapenda kushiriki watatakiwa kufungua akaunti ya FINCA, ambao pia watatakiwa kuweka kiasi cha TZS 20,000 (Salio jipya katika akaunti zao) Watatakiwa kujaza fomu katika matawi ya FINCA ambapo watabainisha katika fomu hizo kuwa wataenda kufanyia nini zawadi hiyo katika biashara zao iwapo wataibuka kuwa washindi.  Baada ya hapo fomu hizo zitawasilishwa katika matawi yetu, mpaka hapo watakuwa wametimiza vigezo vya hatua ya kwanza ya shindano".

"Hatua ya pili, washindani 8 watachaguliwa na jopo la majaji kushiriki katika kipindi cha TV ambacho kitajulikana kama ‘Kuza Ofisi na FINCA’ kitakachokuwa kinarushwa kupitia TVE.  Mwishoni mwa shindano, mshindi mmoja mwenye bahati ataondoka na zawadi nono ya zaidi ya TZS milioni 10", Alisema Nicholous, akiongeza kwamba washiriki wengine wenye vigezo pia watakuwa na nafasi ya kujipatia mikopo kutoka benki hiyo. 

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Biashara wa benki ya FINCA Microfinace Benki, Emmanuel Mongella amesema:  "Kampeni ya Kuza Ofisi na FINCA ni sehemu ya FINCA kusherehekea miaka 20 ya uendeshaji wa shughuli zake nchini Tanzania ambapo benki ya FINCA imekuwa maarufu kwa utoaji wa masuluisho bora na aina mbalimbali za akaunti, Mikopo na huduma zingine ambazo zinajumuisha mahitaji ya watu binafsi na taasisi."

Mongella pia aliongeza kuwa "Ushirikishwaji wa Kifedha na Uvumbuzi wa Kidigitali ni msingi wa biashara yetu, Shindano hili ni ahadi nyingine ambayo Benki ya FINCA Microfinance inatoa kwa watanzania kwamba iko kwaajili ya kuwasaidia katika misaada ya kifedha kupitia elimu na kuwawezesha wateja wetu kuweza kupata maendeleo endelevu ya biashara zao”. 

"Kwa hiyo tunawakaribisha wamiliki wote wa biashara ndogo ndogo walioko Dar es Salaam kujiandikisha na kushiriki katika shindano kwa sababu shindano hili ni kwaajili yao.  Wateja wote wa Benki ya FINCA Microfinance Banki na wale ambao sio wateja wetu wanapaswa kutembelea matawi yetu ya Dar es salaam kwa maelezo zaidi ambako pia watapatiwa msaada wa mahitaji yote wakati wa kujaza fomu. 

John alisema kuwa "Hii ni nafasi kwa wamiliki wa biashara ndogo walioko Dar es salaam kuchangamkia fursa hii adimu na kuja  kufungua akaunti na kushiriki katika shindano ili waweze kuwa washindi wa zawadi ambazo zitakuza biashara zao"

No comments:

Post a Comment

Pages