BALOZI wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Simon Mumwi, leo
ameendesha semina kwa wamiliki wa Kampuni ya Usafirishaji (Tour Guard)
mjini Moscow ili kuwapa ufahamu wa vivutio mbalimbali vya utalii
vilivyopo nchini Tanzania.
Semina hizo ambazo hufanyikanyika mara moja kila mwezi, zinalenga kuongeza idadi ya watalii kutoka Urusi na nchi za jirani.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Balozi Mumwi, alisema kuwa semina hizo zimekuwa na
manufaa makubwa kwani katika kipindi kifupi zimesaidia sana kuongeza
idadi ya watalii wanaotoka Urusi kwenda nchini tanzania, ambapo alisema
"katika kipindi cha miaka 10, idadi ya watalii kutoka nchi Urusi
imeongezeka kutoka 1500 mpaka 15,000 mwaka huu."
Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Simon Mumwi,
akinzungumza wakati akifungua semina na siku moja ya kuhamasisha utalii
wa Tanzania nchini Urusi, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Ubalozi, 51 Ulitsa Bolshaya Nikitskaya, Jijini Moscow, nchini Urusi. wanufaika wa semina hiyo walikuwa ni waendeshaji wa huduma za Utalii nchini Urusi.
Balozi
wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Simon Mumwi, akifuatilia mada ya
utalii nchini Tanzania, iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Kampuni
ya Safari ambaye ndiye aliyewezesha kuwakutanisha wadau wa masuala ya
utalii nchini Urusi, Galina Modestova (kushoto) aliyekuwa akiwasilisha
mada hiyo kwa lugha ya kirusi.
No comments:
Post a Comment